Ahadi ya kukutana na Mupenzi

Mmepeana ahadi ya kukutana na mpenzi ME/KE na mkakubaliana time rasmi ya kukutana mahali hapo. Mpenzi kachelewa kufika je utamsubiri kwa muda gani kabla ya kuamua kuondoka? Utakapoamua kuondoka utampigia simu, kumtumia text message at whatsapp kumfahamisha kwamba umemsubiri hakutokea hivyo umeamua kuondoka?

Mie nitasubiri nusu saa na nikiondoka sitampigia simu, wala kuandika text message au whatsapp kwani tabia za kutoheshimu muda wa mtu mie zinanikera sana. Ukipenda unaweza kuita tabia za kiswahili swahili.

https://www.youtube.com/watch?v=0RyInjfgNc4

Sio kwa mpenzi tu tabia yakucheleweshana haifai kabisa. Waafrika wengi hatuthamini muda kabisa

Hilo nalo neno Mkuu, Waafrika wengi hawathamini kabisa muda. Kuchelewa kwao kwa mambo yenye umuhimu mkubwa wanaona ni jambo la kawaida kabisa na wengi wao hawajali hata kuomba samahani kwa kuchelewa.

Masaa 2 nitamsubiri, nikiondoka lazima nimchambe

Dah! Mkuu weye una moyo kweli wa uvumilivu. 2 hours!

ndio mkuu utafanyaje sasa si mpenzi wako na unampenda

Ni kweli Mkuu ila mie siwezi kusubiri baada ya nusu saa na wala simtafuti nitasubiri uongo wake inawezekana kabisa ana sababu ya msingi ya kuchelewa.

Sheikh kama ni makutano kwa ajili ya kula mzigo! Ntachoma tu Mahindi

Oh! sawa Mkuu hilo la kula mzigo wala sikuliweka akilini Mkuu lakini kama ni kula mzigo nakubaliana nawe Mkuu lol!

Inaumiza sana msipoonana

Haaaahaaaa. Unasusa kabisa

Hahahahaha lol! Hivi kufanya hivyo ni kususa Mkuu? Wahenga si walisema ahadi ni deni? Au ni aje Mkuu?

Unavumilia tuu kama kweli unamhitaji, maana hujui mwenzio kapatwa na nini.

Na mvumilivu hula mbivu

Mimi huwa najali sana muda, na siwezi msubiri mtu zaidi ya dk 10. Nikiondoka nitamtex tuu kuwa naondoka! Huwa naonaga ka dharau fulani hivi

Mh! 10 minutes only!? That’s so harsh Sakayo!!! What if he was stuck in traffic due to one reason or another?

0-1 England

[emoji91] [emoji91]

Kabisa Mkuu

1-1 dakika ya 67