Ahsanteni Kenya Talk bado tuko pamoja huku ni nyumbani pia

Ingawa Jamii forums imerudi hewani bado nitaendelea kuwaungeni mkono ndugu zangu
wa Kenya talk kwa kutukaribisha vema na kutupa Jamvi la kuongelea kwa uhuru Mkubwa
Kabisa, bado hata hapa ni nyumbani na tutaendelea kufanya kuwa makazi yetu kwani tumetanua
Wigo wa kufahamiana kitabia. Sasa nimeanza kuwaelewa wakenya kiasi na nafahamu kwa siku za usoni
Tutakuja kushirikiana vema zaidi.

hapa sijaelewa, najua kuna tv za sony na radio za sony, lakini sijawai skia siku za usoni

bado tupo tupo

bado tupotupo huku hatuondoki ngo

Aisee!

sure, bado tupo sana!

Ana maana ya ‘Siku zijazo’

Hapo sawa kabisa

Inapendeza…

Cc: @Mahondaw

Siku zijazo/ siku za mbele/ siku zinazokuja/ siku zinazofuata.

Ha ha ha ha ha Ni shiida.

Hapa ni home. Kule kwetu hawakawii kuchezea kwenye matukio muhimu.

Hii ni nyumba ndogo

Shukurani ndugu zetu wa Kenya kutupokea in the hour of need. A friend in need is a friend indeed. Mungu ibariki Afrika Mashariki na watu wake.

Hakika hii ni busara kubwa

Kila sehemu kuna ladha yake, ila huku unakuwa huru zaidi…

Mpka nitakapoamua vinginevyo kwa sasa JF nimeamua niwe mgeni nasoma tu habari na kutulia

Tupooo

Bado tupo

Yeah, bado tupo sana. Wakenya ni watu wazuri sana na wanatupenda sana watanzania.