Ahsanteni Moderators wa KenyaTalk.

Napenda nitoe pongezi za dhat kwa uongozi wa Kenyatalk kwa kutukaribisha sisi wana JF kwa moyo wa dhati kabisa, mumeonesha uungwana sana.

Kwa sasa naona metuwekea majukwaa yetu pendwa ya JF ndani ya Kenyatalk, ambapo naweza kuiita JF ndani ya Kenyatalk.

Huo ndio upendo wa dhati kwa jirani yako katika kipindi cha shida na raha, tupendane na tushirikiane ipasavyo wote Wakenya na Watanzania katika hii Forum ili tuweze kuelimisha, kupashana habari mbalimbali katika nchi zetu na kidunia kwa ujumla.

Ahsanteni sana.

Nimefurahi sana kuikuta Jf huku. Asanteni sana jirani zetu wa Kenya kwa moyo huo

Vipi?kuna jamii forums kwa twitter?

Hapana mkuu

Walikuwa na page tu kama zilivyopage/account zingine za mtu mmoja mmoja

Asanten wakenya kidogo nimeshusha pumzi

Serikali ya tz imefanya jambo la kishenzi sana.

Nime fanya utafiti nime pata handle yao twitter [ATTACH=full]175465[/ATTACH]

Karibu,vipi hii ndo id yako kule au?

Hiyo ndio page yao kama nilivyokueleza, hata mimi nimewafollow.

Kuna page zao zingine za FB na Instagram pia

Wamezingua sana aisee

Sijui na huku watafuata wafute hii forum? Ningefurahi kama members wengi wa Jf wangekuja huku kupunguza hasira zaoza kufungiwa tikajadili mustakabali wa sheria hii kandamizi

Huku hawawezi kuja maana ipo nchi nyingine

Ningefurahi kama members wengi wa Jf wangekuja huku kupunguza hasira zaoza kufungiwa tikajadili mustakabali wa sheria hii kandamizi

Mimi wale nilionao mawasiliano nao nawaalika waje wajiunge huku na wao watawaalika wengine hatimaye tutajaa kama ilivyokuwa JF
[/QUOTE]

Kushindana na teknolojia ni ushamba wa hali ya juu Haya sasa tupo Jurisdiction nyingine Mambo yanaendelea.

Ngoja tumuachie nchi yake ila makombora kama kawaida tutarusha kutoka huku huku

[FONT=tahoma]Mada moto moto tunazisubiri waalikeni wadau walioko fb waje humu jamani hima[/FONT]

[FONT=tahoma]Sema modes wa humu naona kama hawako faster wadau.[/FONT]

Tuwaalike wale waliokuwa JF, kama unamawasiliano nao hata mmoja unamualika na yeye ataalika mwingine, kwa mtindo huo tutajikuta tumealika wengi

asante mungu na pia asanteni ndugu zetu wa kenya kutupa hifadhi ,walaaniwe wote walioifunguia jf ya tz ,kesho natoa vipeperushi chuo kizima na kwenye magroup yote ya whatsapp kuwaambia watu kua jf inapatikana hapa

Itakuwa jambo jema sana mkuu

[/QUOTE]

Tangujana nimealika wengi pia, watajua tuu nadhani ndani ya wiki 1 wake zangu Inna, Demiss, Mbitiyaza Miss Natafuta, Miss chaga nk watakuwepo hapa