Alfajiri ya kupendeza (Happy new year)

SIKUKUU YA BIKIRA MARIA MAMA WA MUNGU

JANUARI 1

Somo I: Hes 6:22-27

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia; Bwana akubarikie, na kukulinda; Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani. Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia.

Zab: 67:2-3, 5, 6, 8

  1.   Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake. Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote. 
    

(K) Mungu na atufadhili na kutubariki

  1. Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani. (K)
    
  2. Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru. (K)
    
  3. Nchi imetoa mazao yake MUNGU, Mungu wetu, ametubariki. (K)
    
  4. Mungu atatubariki sisi; Miisho yote ya dunia itamcha Yeye. (K)
    

Somo II: Gal 4:4-7

Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.

Injili: Lk 2:16-21

Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini. Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto. Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji. Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake. Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa. Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.

“Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia,” Hes 6:27

“Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,” Gal 4:4

“Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu,” Gal 4:7

“Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini,” Lk 2:16

“Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake,” Lk 2:19

“Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa,” Lk 2:20

“Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba,” Lk 2:21

Tumsifu Yesu Kristo!

“Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu,” Mt 5:48

Tusali: Ee Yesu Mwema, niongoze katika kweli na haki. Amina

Happy New Year 2017.

4 Likes

last time nilienda church was two thousand and…even forgot.

1 Like

Happy new year

1 Like

Happy New Year to all villagers
Let’s go to church and dedicate the New year to God

1 Like

Sifa kwake ewe Kristu

1 Like