ALI KIBA ACHAMBUA UDHAIFU WA HOJA ZA MWANASHERIA MKUU SWALA LA EXPORT LEVY YA KOROSHO

By Ali Kiba

SIKUBALIANI NA MAJIBU YA MWANASHERIA KUHUSU SERVICE LEVY YA KOROSHO.

Mwanasheria Mkuu (AG) wa Serikali, Dr. Kilangi, gwiji na mbobezi wa sheria ninayemheshimu sana tena sana lakini sikubaliani na majibu yake kuhusu swala la Cashewnuts Export Levy. AG ametoa hoja kuu 3 za kisheria lakini nitafanya uchambuzi wa hoja moja tu ili nisiwachoshe kusoma maana mimi huwa ninaandika kurasa nyingi sana linapofika swala la sheria ninaweza kuchambua hoja zingine mbili iwapo wajumbe wa jamvi hili watataka hivyo. Hoja ya AG ni kama ifutavyo ”Makusanyo yote ya cashewnut export Levy in fedha za umma na serikali ndo ina mamlaka ya kuamua matumizi ya pesa hizo”.

MSIMAMO WANGU.

AG anasema kuwa kwenye kesi ya Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund Vs Cashewnut Board of Tanzania , Civil Appeal No. 18 of 2001 Mahakama ya Rufaa iliamua kuwa Makusanyo yote ya cashew nut export Levy (CEL) in fedha za umma na serikali ndo ina mamlaka ya kuamua matumizi ya pesa hizo, na huu ndo msimamo wa kisheria kwa sasa. Niukata msimamo huu wa AG kwa sababu kuu nne.

Kwanza, mwaka 2010 the Finance Act, 2010 ilibadilisha msimamo wa kisheria (legal position) uliokuwepo wakati na baada ya Kesi tajwa kufanyiwa uamuzi na Mahakama ya Rufaa. Section 4 of the Finance Act, 2010 iliifanyia mabadiliko the Cashewnut Industry Act, 2009 na kuongeza Kifungu cha 17 A (2) (a) and (b) ambacho kimeifanya asilimia 65% ya Cashewnuts Export Levy kuwa ni fedha za Cashewnuts Industry Development Fund na kuifanya asilimia 35% kuwa fedha za umma na ndo maana sheria inasema 65% ziwekwe kwenye mfuko binafsi kwa sababu sio pesa za umma na ndio maana sheria inasema 35% ziwekwe kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali ( Consolidated Fund) kwa sababu 35 % ni pesa za umma. Pesa za umma lazima ziwekwe kwenye Mfuko wa Serikali au kwenye mfuko ulionzishwa na sheria ya bunge au na Waziri wa Fedha, hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 135 (1) na (2) ya Katiba ya JMT na Vifungu vya 11 na 12 vya the Public Finance Act, 2001, hivyo, ni marufuku kisheria na kikatiba kuwe pesa za umma kwenye mfuko binafsi ambao haujaanzishwa na sheria au katiba au waziri wa fedha. Hivyo basi, kwa sababu sheria imeelekeza 65 % za CEL ziwekwe kwenye Cashewnuts Industry Development Fund ambao sio mfuko wa umma bali ni mfuko binafsi basi 65% za CEL sio mali ya umma bali ni mali ya Cashewnuts Industry Development Fund.

Pili, AG alisema bunge kwamba Mahakama ya Kuu katika kesi ya Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund Vs Cashewnut Board of Tanzania, Civil Case No. 204 of 1999 iliamua kuwa ”Makusanyo yote ya cashewnut export Levy in fedha za umma na serikali ndo ina mamlaka ya kuamua matumizi ya pesa hizo”. Ni kwa bahati mbaya sikuweza kupata nakala ya uhumu ya Mahakama kuu, hatahivyo, kama kauli ya AG ni kweli kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu basi uamuzi huo wa kwamba Cashenut Export Levy ni pesa za umma ulitenguliwa na Umauzi wa Mahakama ya Rufaa katika Civil Appeal No. 18 of 2001 ambapo Mahakama ya Rufaa ya Rufaa katika ukrasa wa 18 wa hukumu iliamua kuwa cashewnuts export levy ni pesa za wakulima na sio pesa za serikali kwa sababu levy sio kodi (tax revenue), ninanukuu uamuzi huu wa kama ifuatavyo;

“Whatever the case, the cashewnut export levy money was not revenue from taxation so it was not, and is not government revenue. Ordinarily the money would belong to the cashewnut farmer.”

Mahakama ya Rufaa ina mamlaka kikatiba na kisheria ya kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, rejea Ibara ya 117 (3) ya Katiba ya JMT na Kifungu cha 4 cha the Appellate Jurisdiction Act, 1979. Pia Kunga ya kisheria ya Stare Decisis inaelekeza kuwa iwapo uamuzi wa Mahakama ya Rufaa una nguvu dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu na iwapo kuna mkinzano basi umuzi wa mahakama ya Rufaa ndo utachukuliwa kuwa halali kisheria na hule wa mahakama kuu utakuwa batili kwa kiwango unachokinzana na uamuzi wa Mahakama ya Rufaa. Kunga ya inatambuliwa na Kifungu cha 2 (3) cha Judicature and Application of Laws Act, Cap. 358 na katika kesi ya NBC Limited Vs Kalunga & Company Advocates, Misc. Civil Application No.225 of 2004 Mtukufu Jaji Kiongozi, Manento katika ukrusa wa 5 aliamua kuwa Stare Decisis ni kunga takatifu ya kisheria katika mfumo wa sheria wa Tanzania, hivyo Mahakama zote ikiwemo Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa Hazinabudi kuheshimu kunga hii.

Tatu, for the sake of argument only, hata kama Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund Vs Cashewnut Board of Tanzania, Civil Appeal No. 18 of 2001 ingelikuwa imeamua kuwa export Leavy ni pesa za serikali bado 65 % ya pesa za export levy haziwezi kuwa pesa za serikali hii ni kwa sababu uamuzi huu ulifanywa mwaka 2006 miaka 4 kabla ya the Finance Act, 2010 kutungwa na the Finance Act, 2010 ilipotungwa ilibadilisha msimamo wa kisheria wa awali kama ambavyo ungelikuwa umetafsiriwa na mahakama ya Rufaa kwenye kesi hii kwa kufanya 65 % ya CEL kuwa fedha binafsi za Cashewnut Industry Development Fund. Hivyo basi, uamuzi wa Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund) Vs Cashewnut Board of Tanzania ungelichukuliwa kuwa UNAKINZANA na Kifungu cha 17 A (2) (a) and (b) cha Cashewnut Industry, 2009 kama kilivyofanyiwa mabadiliko na Kifungiu cha 4 cha the Finance Act, 2010. Kwenye kesi ya NBC Vs Jackson Nahimawa Sinzo Bakwila [1978] LRT 38 iliamuliwa kuwa iwapo uamuzi wa mahakama UNAKINZANA na Sheria iliyotungwa na bunge basi uamuzi huo ni batili kisheria na sheria ya bunge ndo itachukuliwa kuwa halali kisheria. Kwa lugha ya Kiingereza tunasema Where case law is at variance with the statute the later prevails over the former and the former perishes to the extent of variance Hivyo basi, uamuzi wa Mahakama ya Rufaa katika kesi ya_Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund Vs Cashewnut Board of Tanzania_, ungechukuliwa kuwa batili na kutokuwa na nguvu ya kisheria kwa sababu ya ukinzani wake na Kifungu cha 17 A (2) (a) and (b) cha Cashewnut Industry, 2009.

Nne, Mahakama ya Rufaa kwenye Kesi tajwa hapo juu (Civil Case No 18 of 2001) ili tafsiri Export Levy ya kiwango cha 3 % of F.O.B ambayo uwepo wake ulisababishwa na Section 8 and 29 of the Cashewnut Board of Tanzania Act, 1984 na Rule 21 (1) the Cashewnuts Marketting Regulations, 1996 (G.N. 369 of 1996). Mahakama ya Rufaa hakutafsiri na haijawahi kutafsiri Cashewnuts Export Levy ya kiwango cha 15 % of F.O.B ambayo uwepo wake ulisababishwa na Kifungu cha 17 A (2) (a) and (b) cha Cashewnut Industry, 2009 kama kilivyofanyiwa mabadiliko na Kifungiu cha 4 cha the Finance Act, 2010. Hivyo basi, kesi ya Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund Vs Cashewnut Board of Tanzania, Civil Appeal No. 18 of 2001, kwenye swala hili ni irrelevant na haihusiki kabisa.

Huu ni mtizamo mtizamo wangu kama mwananchi wa kawaida mwenye uelewa mdogo kwenye maswala ya sheria, hivyo mtizamo wangu unaweza kuwa sahihi au ukawa sio sahihi yaani ukawa na makosa,.

Ali Kiba??

Ndio Ali Kiba.

yupi huyo? wa mvumo wa rad?

Ilishaletwa humu halafu mmeambiwa Ali Kiba hana uwezo wa kuandika hizo nondo.

Hii ni nyingine, ambayo ilishaletwa humu ni hile inayo husu uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh kuwa mwenyekiti wa TEITI, hii ni mpya kabisa inahusu export levy ya korosho.

Mkuu wewe ndo hua una shuka hizi nondo?

ALI KIBA huyuu tulieotoka nae kuanzia kwenye nyimbo ya Cinderella

Ali Kiba tena!!

Kama hii imeandikwa na Ali Kiba basi hata ile misemo ya ajabu itakuwa inaandikwa na Mugabe…

Alikiba hana uwezo wa kuandika haya.

nondo nzur nmejifunza kitu bt jmn alikiba na siasa wap na wap, yuko makin na kaz yake hapo katumika tu

ali kiba huyu hapana labda kaandikiwa na mkewe maana msomi

mheshimiwa zito atumiwe nakala hii ya nondo nzito kutoka kwa ali kiba (wa KT?)

Ukiwafuata CCM hata kama una akili kuliko Plato jua mwisho wa siku utajigeuza zuzu. Hili bandiko limenifanya nione ni kwa jinsi gani CCM wanacheza na akili za watanzania. Hongera Ali Kiba na nadhani ulikuwa unaandika huku unasikiliza wimbo wako wa “Seduce Me!”.

Yupi yule kidoti. Kidoti si aliachana nae

Hawezi kuchambua mavitu makubwa hivyo, hapo atakuwa ameandikiwa na mwanasheria!

bila kujali[SIZE=7][COLOR=rgb(41, 105, 176)] uwezo [/SIZE]wake je kilichoandikwa???[SIZE=2][COLOR=rgb(65, 168, 95)]kwa uwezo wako unepata chochote[/SIZE][SIZE=7][COLOR=rgb(61, 142, 185)]“”“”“”“”
[COLOR=rgb(61, 142, 185)][ATTACH=full]180379[/ATTACH][/SIZE]

@Abeto Malakoti mwambie Ali Kiba amalizie na zile hoja zingine mbili. Nimefurahia sana matumizi ya Kiswahili fasaha na umahiri wa kujielezea alio nao!

Niko naye kwenye group moja la WhatsApp linaitwa CRITICAL THINKER, kila aki post kitu mimi ninawaletea uku ukimbizini Kenya Talk. Jana kamchana Habibu Mchange kwenye hoja ya korosho baada ya Mchange kuandika walaka mrefu kuhusu swala la export levy ya korosho, na hii ya kumchana Habibu Mchange niwaletee?