Asilimia 95% ya wana Jf tulio humu hatujawahi kufungua Majukwaa ya Kenya talk.

Salaam.

Tangu Jf kupigwa Bann pale home Tz na kuamua kuja kujihifadhi huku Kenya chini ya mwavuli wa Kenya talk wadau tumekuwa busy na majukwaa yetu ya Jf tuu…

Kenya talk ina mwajukwaa mengi tuu lakini sidhani kama tumewahi kufungua hata moja zaidi yaku browse direct to the JamiiForums nakuingia Habari na hoja mchanganyiko Mara Jamii intelijensi na mengine.

Kama utafiti wangu si wakweli hebu niambie wewe umewahi kufungua majukwaa mangapi ya Kenya talk tangu Uingie huku,? naamini utaanza Leo baada yakusoma Uzi huu.

Kweli hapa ni habari na hoja mchanganyiko

Mie hayo majukwaa yao hata siwaelewi nawaza hiki ni kiswahili au kijaluo sielewi maneno yao

Uko sahihi mtoa mada

Licha ya kutoelewa sheng, bado hakuna hoja constructive kama tulizozizoea jf! Yaan mtu anaandika uzi una sentesi moja au mbili kamaliza!

Huwa nafungua na kukoment jukwaa la kenya sports hata uzi nimeshaanzisha huko

Sema wewe ndio huingiagi mkuu.

Wabongo tunaingia sana kwenye majukwaa yao hasa ya udaku na mapenzi.

Mimi huwa napita pita huko, huwa nawaona dada zetu huko.

labda wewe ndio uingii huko usiwasemee wengine Mimi huko naingia na nyuzi kama kawaida tuweka

Mtu anaandika

Colombia vs Japan.-hiki kichwa cha uzi

Halafu anaandika “mnasubiri mimi niandike”

Hapo uzi ushakamilika

Mimi nimejiunga huku kabla Jiwe hajatusukumiza.

Majukwa yao nayatembelea sana na hadi sasa nina nyuzi kadhaa kwenye majukwaa yao

Mimi huwa napita tu kusoma comment zao za kiswahili mix na kiingereza basi zinanifurahisha sana

Sijawahi kwenda na wala sifikirii kwenda
Mkimbizi mtata

Sex And Relationship
Ili Jukwaa Lao Nipo Available Daily

natembelea majukwaa machache sana ya wakenya

Ni kweli. Tatizo kilugha chao

m ndo kwanza nimejiunga hii asubuh hata ku comment siwez

Kumbe KT ina majukwaa yake mengine tofauti na haya yetu?

Nilikua sijui mimi

Aisee

Hujui kama hii sub forum yetu imetengenezwa baada ya sisi kuzimiwa JF yetu home, wadau walipokuja huku ndio wakaomba kutengenezewa sub forum maana ilikuwa ni vigumu kujadili na wakenya kwa kiswahili chao tata

Hahah!! Bora imekua hivi mana jamaa wanajifanya wajuaji sana pia wana matusi mno tusingewezana

Ndicho kilichotufanya tuombe sebule yetu pembeni