Baba Diamond amvaa Baba wa Ommy Dimpoz amwambia aache shobo lasivyo atapata tabu sana

Baba mzazi wa Staa wa Bongo fleva Ommy Dimpoz, Mzee Faraji Nyembo amemtolea povu Baba wa staa Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma kutokana na tabia yake ya kumsema mwanaye vibaya.

Gazeti la Risasi Mchanganyiko linaripoti kuwa Kwenye mahojiano waliyofanya na Baba Ommy Dimpoz alitoa taarifa ya mtoto wake kuendelea vizuri na kusisitiza hata kama mtoto wake hamsaidii kwa lolote maishani lakini hawezi kumsema vibaya kama Baba Diamond anavyofanyaga kwa mwanaye.

Unajua mimi ni mzazi wa tofauti sana, siwezi kumlalamikia au kumsemea mabaya mwanangu kwenye vyombo vya habari kama anavyofanya baba Diamond, ninachofanya huwa namuombea mwanangu awe na maisha mazuri maana nikimuombea mabaya anaweza kupoteza dira ya maisha yake nitakuwa nimefaidika na nini.

Namshauri baba Diamond awe anamuombea mwanaye mafanikio, aungane naye wawe kitu kimoja, afurahie mafanikio yake ipo siku Mungu atamrudisha kwake amsaidie na siyo kumzungumzia maneno ya kumlaani na kumlalamikia kila siku.

Aige mfano wangu maana mimi huwa simlazimishi mtoto anisaidie bali huwa napambana na hali yangu kwa kufanya kazi kwa bidii na ninampenda sana mwanangu Dimpoz na siwezi kumlaani au kumlaumu maana jina nililompa la Omary ni la baba yangu inakuwaje sasa nimlaani ni sawa na kumlaani baba yangu”. Baada ya povu hilo gazeti hilo lilimsaka Baba Diamond na kumuhoji kuhusu kile alichosema Baba Dimpoz na alimwaga povu hili:

Sitaki shobo, huyo baba Dimpoz simfahamu kama hana la kuongea anyamaze, amzungumzie mwanaye hata kama niliongea kuhusu Diamond si mtoto wangu yeye inamuhusu nini?”. Kuhusu huyo Diamond sihitaji kuzungumza chochote kuhusu yeye wala watoto wangu maana hawana faida yoyote kwangu kwa sasa”.

Wototo kiki, wazazi kiki, kizazi kijacho kitapata tabu sana…

MaKiK hadi kwa wazee… aisee

asee kumbe ht omi dimpoz hamsaidiai mzee wake! sawa baba tumekusikia

Wanaume wa Dar mnakazi kweli kwa maneno mnaweza msema mtu mpaka akazimia!

Wababa wa mjini hao,wanachambana kwenye magazeti

Waandaliwe mpambano wa ngumi wamalize ubishi, wasilete maneno maneno kama mademu.

Wababa wa dar

Hawa wazee nao mh

Hawa wazee wangejua wanavyofaidisha haya magazeti wange kaa kimya tu.

If u think small u’ll remain small for a life

“gazeti la risasi”