Bajeti ya Tanzania 2018/2019 kusomwa leo jioni.

Waziri wa Fedha na Mipango wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Philip Mpango anatarajia kusoma bajeti ya Tanzania 2018/19. Ni kuanzia sa 10 Jioni leo hii, TBC 1 itakuwa Live kwa watakaopata nafasi ya kufuatilia.
Bajeti hiyo itatoa mwelekeo wa uchumi kwa mwaka 2018/19.

ngoja tuisubiri nilianza kumiss uchambuzi wa JF

max inabidi arudi hewani chap tukaichambulie nyumbani

Haitakuwa na jipya hiyo… Lissu alikiita kipindi hicho “Silly Season”… Mbwembwe nyingi hakuna jipya!! Bahati nzuri leokombe la dunia linaanza!!!

Kabisa. Hivi Mod si anirudishie ile avator yangu maana nimekuja huku ughaibuni sioni avator

leo tuko russia.

Tayari TBC wako live

Hahahahaaaa… Kumbe Mods ndio wanaoweka avatar!..

Tupeni na updates basi jamani,maana wengine tuko mbwinde huku hatujui kinachoendelea…

Mkuu umetuchanganya kusema wanaanza saa 11 kumbe wameshaanza

Kuna jipya?
Au yaleyale ya siku zote?

Russia mechi inaanza saa ngap?

Nipo RUSSIA mkuu, hata wabunge wengine hawajaenda leo wapo Russia itakuwa mimi?

Kweli mkuu, Zungu ameniingiza chakike

Ndo naendelea kujifunza kusikiliza bajeti

Kitu ambacho waziri wa fedha ameshangiliwa zaidi ni kauli yake ya HITIMISHO.
“Anasema Watanzania Mungu ametutunuku Kiongozi bora ambaye ni Dr. John Joseph Magufuli”

wamefurahia mheshimiwa Rais kusifiwa lakni kilichomo ndani sidhani kama wamepata wasaa hata ya kusikiliza…

Kabisa mkuu

Kichwa cha habari hapo juu chahusika. Hivi kuna jipya huko au ni yaleyale ya hatuwezi kusema hadharani???

Kwa mtazamo wangu bajeti hii kama walichokisoma ndio watakachofuata imekaa vizuri.Eneo ambalo wamenivutia ni kupunguza corporate tax kwa wafanyabiashara ,toka 30% - 20%