BASATA yaufungia wimbo wa SUGU

#SIJAISHANGAA_SERIKALI_YA_CCM_KUUFUNGIA_WIMBO_HUU
■Kama wanaingia hotelini na kupima samaki na rula #UNAWASHANGAAJE?
■Kama wanawaagiza trafiki kutulazimishia makosa ili kila trafiki afikishe faini za makosa 10 ili mapato ya nchi yaongezeke #UNAWASHANGAAJE?
■Kama wanazuia Bunge Live na kuruhusu World Cup live #UNAWASHANGAAJE?
■Kama wanazuia mikutano na maandamano yaliyohalalishwa na katiba ya nchi #UNAWASHANGAAJE?
■Kama wanazuia bajeti ya wapinzani isisomwe bungeni #UNAWASHANGAAJE?
■Kama wanazuia mtoto wa kike aliyebakwa/kurubuniwa akapata mimba asirudi shule…

Yaani hii nchi CCM wanapenda sana kujitisha kwa kivuli chao wenyewe!!

Sugu aache ujinga wa kupuuzia mambo. Aende Mahakamani akaombe tafsiri na awalazimishe BASATA wawalete hao watu waliolalamika. Pia kwa barua ya BASATA ni kwamba Sugu anaitwa mchochezi na msambaza sumu kwenye jamii.
Sugu nenda mahakamani.

Naona BASATA wanaupo promo bila kujielewa…sasa ndio wengi watautafuta huo wimbo kwa lazima.

Mimi tayari ninao kwenye simu na jamaa zangu kibao wanao, na tulishaujadili sana ngoja tuanze kuujajidili upya.

Wana matatizo sana hawa

mbona tunao tayari?

Wamefungia usichezwe redioni au wamefungia tusiusikilize?

Tukisema ccm imejaa vichaa watu wanatoka povu.

Kuna kitabu cha The dark side of Nyerere legacy kilipigwaga marufuku cha ajabu watu wakaanza kukitafuta kwa udi na uvumba wajue kina nini na kwa nini kimepigwa marufu.

Yaani unakipa promo kitu kwa njia ya kukikataza.

Watoto ukiwaambia msifanye mapenzi ndio kwanza watajaribu wajue ni nini kilichofanya uwakataze.

!
!
Aisee… Mwenye Huu Wimbo Auweke Hapa Tuushushe

ngoja niutafute! afu basata acheni usoro.

Ni mwendo wa kusifia na kupongeza tu,ukienda kinyume cha hapo jnalula ban…

mwenye nao plllls atupie hapa

Mimi Wakudata nauliza “Eti wajomba kawimbo kenyewe ndio haka hapa kwenye adachmendi?” BASATA siku hizi wamelazimishwa kutumia akili taahira ya jiwe!!

Angalia hapo juu nimeutupia kiongozi wangu!

Duuuh

Tangu huyu mtu aanze kutawala nimekuwa nikijiuliza Tanzania ingekuwaje kama angetawala Enzi zile za radio tanzania?

Aiseeh!! Baada ya kusikia wameufungia huu wimbo imebidi niutafute niusikilize nimeona ni wimbo mzuri sana.

Mimi nilitarajia hili kutokea

https://www.youtube.com/watch?v=P66kumsZu88

Ahsante kenyatalk Ahsante teknoloigia Ahsante Youb Tube Enjoy it

duuuuh