Boing, kunani Boing mwaka huu??

Boeing nyingine yapata hitilafu angani, yalazimika kutua ghafla

Ndege aina ya Boeing 787-900 ya Shirika la United Airlines leo Jumatatu imelazimika kutua katika kisiwa kilicho Bahari ya Pasific cha New Caledonia baada ya taarifa kuwa kulikuwa na moshi unatoka kutoka chumba cha rubani, ofisa mmoja aliiambia AFP.
Ndege hiyo ya shirika la usafiri wa anga la Marekani iliyokuwa imebeba abiria 256 wakisafiri kutoka Melbourne, Australia kwenda Los Angeles, ilitua salama kwenye Uwanja wa La Tontouta ulioko Noumea ambao ni mjini mkuu wa New Caledonia.
“Abiria wanashuka kwa utulivu,” alisema ofisa kutoka Chama cha Wafanyabiashara ambao wanaendesha uwanja huo wa ndege.
“Inaonekana kwamba kulikuwa na moshi unatoka chumba cha rubani.”
Ndege ya shirika la Ethiopian Airlines ambayo ilianguka na kuua watu 157 Machi 10 ilisababisha kuzuiwa kwa ndege zote aina ya Boeing 737 MAX 8 kufanya safari kote ulimwenguni.
Ajali hiyo ilikuja miezi michache baada ya ndege nyingine ya aina hiyo ya Shirika la Lion Air kuanguka nchini Indonesia Oktoba mwaka jana na kuua watu 189, mambo ambayo yaliibua mjadala kuhusu kuruhusiwa kwa ndege aina ya 737 MAX 8 kufanya safari za kibiashara.
Tovuti ya Nouvelles-Caledoniennes (Caledonian News) iliripoti kuwa vifaa vya hewa ya oksijeni vilishajishusha ndani ya ndege kwa ajili ya abiria kuvivaa ili kuvuta hewa safi.
Kituo cha redio cha RRB kilisema hakuna mtu aliyejeruhiwa na abiria watalala siku moja mjini Noumea, umbali wa takriban kilimota 2,700 Kaskazini Mashariki mwaka Melbourne.
AFP

Chanzo: https://mobile.mwananchi.co.tz/Habari/Boeing-nyingine-yapata-hitilafu-angani--yalazimika-kutua-ghafla/1597580-5041024-format-xhtml-ujk7coz/index.html