Ccm mnachokifanya leo hii ni kuhalalisha

  1. Watu kutolipa kodi
    na
  2. Kuwapa uhalali watu competent kuwasaidia watu kukwepa kulipa kodi.

Kumbe

Aiseeeee

Msilikizeni huyu mburula. Na kwa kuwa hakemewi ina maana huo ndio msimamo rasmi wa ccm. Kodi hukusanywa kwa basis of “no fair representation no right to collect tax”.
Kwa mantiki hiyo it is in our BEST interest to avoid paying taxes. Na na-declare kuwa huo ndio msimamo wangu (na kuanzia sasa nitautekeleza) hadi hapo watakapobdilika.

Nimesema basi tusio CCM tusitozwe Kodi!!

Aisee!..

Dhambi kubwa katika nchi zilizoendelea ni kutolipa kodi. Kosa hilo kifungo ni dhahiri.

Lakini kwenye nchi hizo hizo ni dhambi kubwa zaidi kutoza kodi huku ukiwaambia walipa kodi kuwa hutapeleka fedha zozote kwenye maeneo yasiyounga mkono chama tawala.
Nitajie nchi yeyote iliyoendelea ambayo kiongozi wake anaweza kusema kwa siri (achilia mbali hadharani) kinachosemwa na kutendwa na ccm kuhusu kutenga fedha maeneo wanayopingwa. Ukiweza na ukaleta ushahidi nita-post picha yangu hapa nikiwa uchi wa mnyama.

Nimeandika mara nyingi kuwa siasa za kistaarabu zimepitwa na wakati:

  • Mbowe achia nafasi watu wa kwenda na wakati waingie. Huwezi kuingia uwanjani kucheza na watu ambao viatu ndio mchezo na refa anawahamasisha wapige viatu. Tunahitaji zama za undava undava tu! Tunahitaji vikundi vya kazi vya kupambana na wahuni. Vijana wapo wanangoja maelekezo. Liamsheni dude jamani. Mbowe kaa pembeni zama hizi si zako tena!! Ni zama za akina Lema, Lissu, Msigwa, Mnyika Halima. Ndio tiba pekee iliyobaki.
  • Buyungu hawatakiwi na hawatapata kura lakini wamejiandaa kujitangaza! Ukonga vile vile. Monduli ni patamu hapo maanake Laigwanani wameshatoa maelekezo!

Hizi siasa zetu nadhani tumewaachia watu wasio makini kufanya/kufikiri kwa niaba yetu huwezi kuropoka ujinga kama huo kwamba kama hutachagua CCM serikali haitapeleka maendeleo kwenye eneo lako kama ndivyo inapaswa iwe mamlaka husika isilipishe kodi maeneo yaliyochagua vyama tofauti na chama tawala. Halafu hii hama hama nayo naona imekithiri kodi zetu badala ya kwenda kushughulikia maendeleo zinatumika kununulia watu ili wahame vyama vyao ujinga mwingine wa kiwango cha juu pesa nyingi zinapotea kuitisha chaguzi nyingine sababu ya ubinafsi watu wachache.

Yana mwisho wake…

Cc: @Mahondaw