Nimeona sana hili neno likitawala majukwaa mbalimbali. Ninani huyu Chakubanga?
Huyo ni mwenezi wa chama cha magamba, ndugu polepole
Hahahaaa, kumbee! M nilijua ni Chakubanga yule wa kina Chupaki, Polo, Bushiri na Mama Chupaki
Hapana mkuu, kwenye siasa za bongo chakubanga ni slowslow a.k.a mtaalamu wa hesabu za 1.5 trillion
Hahahaa, wabongo wanajua kutoa identifications kwa kila aina ya watu kutokana na matendo yao
Wabongo kwa Nahau na Misemo hatujambo!!
[ATTACH=full]176831[/ATTACH]
Dah! Madini haya sijui umeyafukua wapi mkuu!
Bahati mbaya sana hivi vibonzo vilikuwa kwenye gazeti la Uhuru ambalo kwa sasa hata kulisoma imekuwa ni kichefuchefu!!
Wakati huo ndio lilikua gazeti pekee ambalo lilikua linatumika kutoa muelekeo wa siasa za nchi na kupasha watu habari zilizoharirirwa na kudhibitiwa na chama
mwenda pole pole
hahahaha mtaalamu wa 1.5 trillion shilingi nimecheka sana long live JF
Maktaba yangu nayo si haba
Hahahaaaa, upo vizuri sana mkuu, umenikumbusha mbali sana
Ndio hivyo mkuu, haya madini yote source ni JF, nikiliona nalitunza maktaba for future use
Safi sana kiongozi
hahahaaa, aisee kazi ipo
Ni mzee wa 1.5tr hazijaiva…au mzee wa magazijuto ya 1.5tr
Kipindi hicho mwenge ni tukio muhimu unaliweka kwenye kalenda kabisa. Enzi hizo watu wazima walikuwa wanadate na wanawake wakutanie kwenye sherehe za mwenge. Hili gazeti ndio baadhi ya vyombo vya habari vilivyoweka msingi wa nidhamu za unafiki na woga ndani ya hii nchi