CHURA!

JIFUNZE KWA CHURA

Ukimchukua chura ukamuweka kwenye sufuria la maji kisha ukatenga motoni, kitakachotokea ni kwamba kadli maji yanavyozidi kupata joto chura naye anakuwa na uwezo wa kujiongeza joto la mwili wake. Chura atazidi kutumia nguvu zake kuuongeza mwili wake joto ili kuendana na joto la maji.

Lakini itafika wakati maji yatakapokuwa yanakaribia kuchemka chura atakuwa hana tena uwezo wa kuendelea kujiongeza. Wakati huu chura atafanya maamuzi ya kuruka na kutoka nje ya sufulia ili walau kutetea maisha yake.

Ataruka na kuruka lakini hatafanikiwa kwa sababu atakuwa ameshapoteza nguvu nyingi wakati alipokuwa akijiongeza ili kuendana na joto la maji. Baadaye maji yatachemka na punde tu chura atakufa.

Swali ni Je! Kitu gani kitakuwa kimemuua chura? Wengi watasema maji ya moto ndiyo yaliyo muua chura. Lakini kwa mtazamo wangu ni kwamba kilichomuua chura ni ujinga wake mwenyewe na kushindwa kuamua ni wakati gani sahihi wa kuruka.

Kijana mwenzangu, hebu fanya maamuzi sahihi sasa. Ruka ungali una nguvu zako zote usisubiri mpaka hali iwe mbaya. Ni kweli maisha tuliyonayo yanahitaji kujiongeza kwa kiasi kikubwa sana, lakini angalia usiwe kama chura wa kwenye tungo hii.

Hapa ninachomaanisha ni kwamba hautakiwi kung’ang’ana na jambo moja kwa muda mrefu kiasi cha kupoteza muda wako pasi na manufaa yoyote. Mwisho ukajikuta umepotea kabisa kwenye ramani ya maisha.

Unapaswa utambue kwamba katika maisha kila mtu ana mlango wake wa kutokea, hivyo ni vigumu sana kutoka kupitia mlango ambao hujaandikiwa.

Kazi ya control C na control P.

Ahsante

Miwa niaje

Poa

Hivi ulisema hutoniunganisha na toto moja tamu la kibongo?

Kuwa nao karibu, jenga urafiki wa hapa na pale utapata tu.

Hamna linalishindikana ukiwa na nia ya kulifanya

Punguza ushauri mwingi kaka, nipe through pass nawe

Hakuna jambo linalowezekana kwa urahisi, lazima pawepo na hatua za kupitia ikiwemo kupokea ushauri na hatimaye utalifanikisha.
Kwa hiyo anza kupokea ushauri kwanza ili ukianza kulifanya usipate vikwazo na kwe rahisi kulifanya

Bwana weeee, kumbuka huku Nairobi sio rahisi kupata toto la kibongo ambalo ni kienyeji ndo maanake

Shukrani

Nice one! #kataa kuwa chura.

Ahsante kwa ujumbe mzuri.

Kweli kabisa…

Tatizo binadamu ni wabishi sana…

Cc: @Mahondaw

Sawa

Kumbe na wewe huwa unakuja huku kuchungulia. Ila naona na JF naa wamelegeza masharti.

Uchura hauna deal

Ndio wewe!

Nimekuja Nduki Nikijua Ni Chura Watu :smiley:

dah, ata mimi, nakikata stim kweli

:D:D:D:D:D