Cyprian Musiba

#1
Hivi huyu ni nani? Cyprian Musiba? Mbona analindwa hivi? Juzi kuna mama mmoja kajitokeza kwa tuhuma kuwa ni mtekaji kwa ushahidi wa RB ya polisi! Lakini vyombo vyote kimya.
Kuna haja ya kutii sheria katika nchi hii? Au sheria ni kwa ajili ya wapinzani tu?

East Africa Television (EATV)
13 Aprili 2018 ·
"Yupo mtu mmoja anaitwa Cyprian Musiba anaita vyombo vya habari na kuanza kushtumu baadhi ya viongozi na kutoa maagizo kwamba ningekuwa mimi ningeuwa hata 200, juzi maaskofu wamezungumza ameitishwa vyombo vya habari anasema angeuawa hata 200 hivi nchi hii si usalama wa taifa wapo, nchi hii si ina dola hivi huyu mtu mnamkalia kimya ina maana mnamtuma? Sasa hivi watu wanapotea, watu wanauawa mtu anasimama hadharani anasema ningekuwa ningeuwa mia mbili halafu anaangalia tu hivi na anaandika kwenye gazeti lake wakati Mhe Mwakyembe shemeji yangu unafungia magazeti kwa sababu mbalimbali huyu anatoa matamko kwenye gazeti lake lakini hafungiwi.
Sasa mimi nataka niwaambie kwa sababu watu wamepotea hapa, watu wameuawa hapa serikali mnamsikia Musiba mnakaa kimya na wala hammchukulii hatua mimi nataka nijenge hoja kwamba serikali mnawajua wauaji kwa sababu Msiba anatamka na hamchukui hatua hivyo ni mtu wenu, vinginevyo mje bungeni mtuambie huyu Musiba ni nani na mchukue hatua dhidi yake" :- Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini.
 
Top