Habari za ugenini?
Niende kwenye mada:
Kama mjuavyo kesho ndio sikukuu ya Eid
Nimeshuhudia ugomvi kati ya wake na waume zao baada ya wanaume wengi kushindwa kumudu/kukidhi mahitaji ya familia zao ikiwemo kununulia nguo watoto,viatu na chakula cha sikukuu.
Baadhi ya wanawake wamewakunja na kuwapiga waume zao,wengine wamewanunia na wengine wakakataa hata kutoa chakula cha usiku “papuchi”
Najiuliza hawaoni vyuma vimebana na mambo yamebadikika,hata sisi wengine tunapost mada zetu tukiwa kwenye server za ugenini?
Wanawake please and please mtuhurumie,maisha ni magumu kwa wengi wetu.
Eid Mubarak
Kuna kipind kimoja nilikua nasikiliza kila jionbaada ya ftari, kinasema siku za mwisho wa mwezi wa ramadhan wanandoa au wazazi wanakua na ugomv wanawake wakiongoza
Hivi unajua na kuona kabisa mumeo hana pesa, akaibe? Ifikie hatua tutambue kuna kupata na kukosa s kila siku mtu atapata tu
Eid haiji kwa bahati mbaya,siku zote maisha ni mipango.Lazima tuwe na nidhamu ya kuweka akiba kila wakati kulingana na kipato chetu ili kuweza kumudu matumizi yetu kwa uhakika bila masikitiko na stress