Fact za soka

Juzi baada ya C Ronaldo kusawazisha goli la 3…, walipokuwa wakishangilia kuelekea nje ya Uwanja ilionekana kuna mchezaji mwenzao wa Portugal akiambiwa abaki Uwanjani…, najua ulipitwa na tukio hilo ila endapo kama uliliona na hukujua kwanini alifanya hivyo basi acha nikijuze…

Kwa Sheria za Soka Sheria #8 inaelezea wazi…, Mwamuzi wa mchezo anaruhusiwa kuanzisha mpira endapo tu Timu moja kama haipo kwenye nusu ya uwanja wa wapinzani wao…, kwamaana hiyo kama Portugal wangetoka wote nje ya uwanja kushangilia pasingekuwa na mchezaji yeyote yule kwenye nusu ya dimba la Spain…, Wapinzani wao wangeweza kujipanga fasta na kisheria Refa anaruhusiwa kuuanzisha mpira…
International players licha tu ya kuwa bora uwanjani haya mambo wanafundishwa pia darasani…, Sheria ni muhimu kuzitambua kabla ya kuwa bora kwenye jambo ulifanyalo…, Ubora huja kwa kuzizingatia sheria…[ATTACH=full]177129[/ATTACH]

ONGEZEA NYINGINE UZIJUAZO

Wachezaji wetu wanayajua kweli haya?

Hawajui hio,na mpira ukiendelea wataona wameonewa

Historia kwa Sweden…

Bao la Sweden leo tarehe 18/6/2018 ndilo lao la kwanza kwenye kombe la dunia tangu 2006 wakati Henrik Larsson alipofunga dhidi ya Uingereza.

Eeh! Na refa atapigwa

Wametoa mkosi

Hahahaha kweli

Fact…

South Korea hawakupata ushindi katika mechi ata moja ya WC iliyofanyika Brasil 2014…

Fact…

Timu ya Taifa ya Tanzania haijawahi kufungwa goli ata moja katika michuano ya kombe la dunia

kwa mara ya kwanza mwaka 2002 nchi mbili kwa pamoja zilianda kombe la dunia
S.korea n Japan

Kuanzia fainali za mwaka 1998 FIFA waliamua Fainali za Kombe La Dunia zishirikishe timu 32 badala ya 24 ilivyokuwa kuanzia 1982 na 16 kabla ya h

India iliwahi kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka 1950 lakini walijitoa kutokana na sababu za kifedha na pia kwa sababu wachezaji wake wengi walipenda kucheza soka miguu peku kitu ambacho FIFA hawaruhusu

Fainali za kombe la Dunia.

ndio world cup

Mwanasoka mkongwe wa brazil pele, alijipatia jina hilo la utani lenye maana katika lugha ya kibrazil na kireno “ miguu sita” (six feet),kutokana na kuwa na vidole sita katika kila mguu.

Mwana soka anakimbia kilomita zipatazo kumi (10) katika mchezo mmoja.

Mwanasoka wa kibrazil, Ronaldinho ndio mfungaji anayekumbukwa zaidi kwa kufunga mabao mengi duniani, alifunga mabao 23 akiwa na umri wa miaka 13 tu.

Mnamo mwaka 1998 Radi iliua wachezaji wote kumi na moja (11) wa timu moja na kuacha wachezaji wa timu pinzani wakati wa mchezo nchini DRC na kudhuru watazamaji wapatao thelathini

Mnamo mwaka 1964 simu aliyopokea mwamuzi wa mchezo (refa) akiwa uwanjani huko nchini Peru ilisababisha vurugu iliyopelekea watu mia tatu (300) kufariki.

Washabiki wa soka nchini Columbia waliingia na jeneza uwanjani la mshabiki mwenzao aliyeuawa kwa kupigwa risasi siku ya kuwania kuingia fainali akiwa na umri wa miaka17. Washabiki hao waliingia nae siku ya fainali.

Mnamo mwaka 1966 kombe la dunia liliibiwa na baadae mbwa akalipata siku chache kabla ya mshindano hayo kuanza. Kombe la dunia kwa mara ya kwanza lilitengenezwa kwa makaratasi na kubadilishwa baada ya kuharibiwa na mvua kali iliyonyesha. Siku hizi kombe hilo linatengenezwa na zahabu yenye uzito upatao kilo 4.97.

Pele alipokwenda Nigeria kucheza soka katika mchezo wa hisani mnamo mwaka 1967, pande mbili zinapigana vita, zilikubaliana kusimamisha vita kwa muda wa masaa 48.

Mrtinho Eduardo Orige kutoka Brazil ndio mchezaji pekee kuchezea mpira kwa muda mrefu zaidi duniani! Alichezea mpira kwa muda wa masaa 19.5, alivunja record hiyo mnamo mwaka 2003.

Ahsante sana mkuu kwa kunifungua macho,hili nilikuwa silijui.
Nalog off