Unaweza usielewe pale mtu anaposema nataka kula embe Sakua, wengi wetu tumezoea kuliita ‘embe ng’ong’o’.
Tunda hili ni miongoni mwa yenye viini lishe na vitamini A, C, beta carotene, madini ya potassium na magineziamu.
Mbali ya tunda hilo kuwa na viini lishe, pia linakiasi cha sukari ya asili aina ya fructose na glucose ambazo huupatia mwili nguvu.
Ulaji wa maembe ng’ong’o mara kwa mara unaweza kukuepusha kupata vidonda vya koo kwa sababu tunda hilo lina vijiua sumu.
Kwa mujibu wa Jarida la Asian Pacific of Tropical Biomedicine lililochapishwa mwaka 2013, linasema sharubati (juisi) ya embe ng’ong’o huongeza hamu ya chakula kutokana na uwezo wake wa kusisimua vitu vya maonjo katika ulimi.
Moja ya faida za tunda hili husaidia kupunguza hatari ya kupata saratani.
Pia ulaji wa embe hilo mara kwa mara husaidia damu isigande kwenye mishipa.
Unywaji wa sharubati ya tunda hilo hupunguza pia uwezekano wa mtu kupata unene wa mwili wa kutisha na kuwa ni kero.
Hivyo, inashauriwa, familia zitumie zaidi tunda hilo kwa ajili ya kujenga afya na kuzuia baadhi yamaradhi kama hayo ya saratani kama inavyoelekezwa na wataalamu wa tiba lishe.
tukumbuke si kila ugonjwa unaweza kutibiwa na dawa za hospitali tu, bali hata vyakula na matunda ni tiba tosha.