Fufua nyuzi yoyote ya jf tuendeleze

Kama kichwa kinavyojieleza nadhani ni wakati wa kufufua nyuzi yoyote unayoikumbuka ili tuendeleze mijadala hivyo usiumize sana kichwa kuanzisha nyuzi mpya…ingawa nyumbani korosho zimeleta balaa

Mkuu korosho zimeleta balaa gani tena???

Vipi wamewachakachua wakulima?

Sakata la korosho limemtisha Spika wa Bunge kiasi cha kutishia kuwa Bunge litavunjwa na Raqis kama wabunge hawataipitisha bajeti… Kina Nape/ Bwege wamezua balaa bungeni…

Wanataka tuendelee kuwa Masikini milele, korosho zetu wazile bure

Swala la Korosho Limepunguza sana Kupendwa kwa Mtu fulani hasa mikoa inayolima Korosho…!!! sijui atafanya nini kurudisha Imani iliyofifia…!!! Hivi ni ugomvi gani usioisha kati yake ''Nahako", ‘‘Napedimbe’’ na ‘‘Liyanga’’ wewe ‘‘Liyanga’’ wape hao watu Nafasi tena wakufanyie kazi…Watu wa KUSINI hawafurahishwi na ugomvi wenu kwa sababu wote ninyi ni wao na wana Matumaini nanyi…