FUNZO KUTOKA NGE!

KISA CHA NGE NA MZEE.

Niwasalimu wa bush wenzangu!

MZEE mmoja aliona nge akitapatapa kuzama kwenye maji. Imani na roho ya kusaidia ikamjia, akaingiza mkono majini ili kumhami. Alipomgusa tu, nge akamgonga. Maumivu aliyoyapata, alijikuta akitoa mkono bila kumuokoa.

Pamoja na maumivu ya sumu ya nge, mzee alipotupa macho tena majini, alimwona nge akizama na kuendelea kutapatapa.
Haraka aliingiza mkono ili kumsaidia. Na kama awali, nge akamgonga tena na kumwachia maumivu makali.

Kijana aliyekuwa amesimama kando, alimuuliza mzee: “Kumradhi mzee, naona kama utadhurika bure. Hivi huoni kila unapojaribu kumsaidia, naye anazidi kukugonga?”

Mzee alijibu, “Uhalisia wa nge ni kugonga, uhalisia wangu kama mwanaadamu ni kusaidia. Uhalisia wangu wa kusaidia, hauwezi kubadilika kama ambavyo uhalisia wa nge wa kugonga usivyobadilika.”

Punde, mzee alichukua kipande cha mti, akakitumia kumuopoa yule nge na kumtoa nje ya maji. Kijana akaandoka kichwa chini, mikono nyuma.

FUNZO: Kamwe usijibadili uhalisia wako. Ukifanya ihsani ukalipwa nuksani, usibadilike.

Badala yake, chukua tahadhari kisha badili mfumo wako wa kusaidia. Hutokea kipindi mtu akakudhuru si kwa makusudi, bali kwa mapungufu yake ya kimaumbile. Kwahivyo, kulipizia uovu ni kujidhulumu nafsi na kujishushia hadhi.

Siku Njema.

Kazi ya Control + C na Control + V

Kaka asante sana pls itabidi uirudie tukirudi nyumbani

Kisa kizuri sana na kina ujumbe mzuri

ujumbe mzuri sana, ila kugingwa na nge na ukarudia tena inataka moyo wa kipekee

Ibilisi

Ndani ya kisa hiki kuna funzo kubwa sana…

Hapa ni kisa cha bwana Jiwe na Watanzania

Kisa kizuri hiki, nimejifunza

Mmemsema Nyumbani! Na bado mnamsema Ugenini!

Sawa kaka. Imekaa powa

Ujumbe maridhawa sana huu…

Tatizo binadamu ni wabishi sana…

Cc: @Mahondaw

Unangatwa kisha unardia…ukakasi

barikiwa saana.

Bado I don’t believe you if you are that guy. Never seen the usual flavour in your stories

Na hasa weww

Kizuri zaidi kama tutazingatia!

Chama kijifunze kupitiaa kisa hiki

CHAMA gani Mkuu? Mana kijijini kwetu kuna CHAMA cha Ushirika, kipo hovyo hovyo

Hahaha mkuu ni Chama cha madikteta uchwara na wakoloni weusi