Fursa kwa undergraduates wasiokuwa na ajira

Wakuu,mimi leo ntatoa ushauri kidogo kuhusu hili janga la ajira.

Wengi wanasema hatuwezi kujiajiri sababu hawana mitaji,sasa basi dawa ya mtaji ni hii
(1) Tafuta soko la vitu vidogo vidogo.
Yani hii maana yake ni kwamba angalia huku mtaani watu wanashida na nini.Anza na vitu vidogo vidogo kama sabuni,chumvi au dawa ya mswaki.

(2)Usikubari kuchukua faida kubwa
Hii maana yake,angalia watu wengine wanapata faida kiasi gani kwa kila bidhaa.Wewe jaribu kupunguza iyo faida ili uuze bei nafuu kwa ubora uleule.Hii itakusaidia sana kupata wateja wengi,na faida utaiona.

(3)WAPI NITAPATA MTAJI
Hapa ndio wengi huwa wanashindwa kuanza biashara kwa kisingizio hiki.
Nini cha kufanya,Anza na mtaji wa sh 5000,uzungushe kidogo kidogo.
Hii elfu 5,ni kama chambo cha kuaminiwa.
KIVIPI
Maduka mengi ya jumla hasa kariakoo,wanatoa sana Mali kauli,ila mpaka uonyeshe uaminifu.
Unaanza kukopa kidogo kidogo mpaka unaanza kupewa mzigo mkubwa.
YOTE 9, CHA UMUHIMU NI UAMINIFU.

Wanasubir dream job wakati muda si rafiki

mie natafuta atakae weza nitafutia masoko ya uhakika wa bidhaa zangu then tunalipana poa poa

Bidhaa gani hizo Mkuu/Villager ,watu wachangamkie fursa?

Kheri wangesoma business administration haya mambo ya uchuuzi tena

Mpaka ueleweke vzr itagharimu muda haswaa,.

Duh mjini shule, God bless wana wote wanaoambana zama hizi za Stone

nipo na kijana wangu tunafuga hawa samaki wa urembo so ka mtu hana mtaji nadhani anaweza nitafutia masoko ya hao samaki namie tutalipana kwa mauzo yaendavyo

Umenikumbusha zamani sana, miaka ya 1993 enzi zile za samaki wa kufuga

kweli mkuu ila bado hiyo biashara ipo tena si ya kitoto ila ya kumtoa mtu yani ka ya njiwa

wow, the first time nawaona hao samaki wa urembo nilidhani ni midoli samaki inachezeshwa kwenye maji aisee, ni wazuri kwa kupambia nyumba, ofisi pia. ila gharama zake vipi, siyo kubwa sana mkuu?

Tuliosoma ualimu tufungue shule?