Hadithi hadithi Hadithi njoo... The story of Miss K

thesavage

Village Sponsor
#1
Hapa wosia wangu nimeutenga kwa wavulana peke yake. Lakini leo nitawashauri wasichana.

Wasichana wengi sana wamekuwa wakishambuliwa hapa kwa sababu ya kutamani makuu mambo ambayo hawafikii. Wanawatenga wale watu wa chini karibu nao kutamani vitu ambavyo hawajui chanzo na hatima yake.

Sawa, hadithi:

Jana, Miss K alitamani kusafiri, lakini alikosa nauli ya kusafiria. She was offered a lift by her long time friend Bwana Beta, akakataa.

Alipokuwa anangojea kukatokea kiairbus a310, akaelekea huko kuomba lift, kumbe limejaa ndege likamwacha. Likaja ndege ndogo aina ya DC twin turbo prop, akaelekea huko kuomba lift akapata pia hilo limejaa. Her long time friend anamwangalia tu.

Tena kachopper kakafika, akaenda pia kuomba lift, akakosa. Mwishowe likaja gari aina ya Rangerover Sport. Mwenyewe akitaka kumpa lift kumbe bibi yake alikuwa ndani akamkataza. Gari likamwacha. Next kasaloon kadogo kakapita pale, aina lake ni mercedes. Akaenda kuomba lift, akapata nadini humo ni boy alikuwa na mchumba wake. Mchumba kusikia miss K anaomba lift akamkataza.

Mwishowe Miss K akarudi tu pale pale kwa Bwana B. Bwana B alipowaza akasema, "Wewe nilikualika lift mimi mwenyewe kwa hiari yangu ukanipuuza. Sasa ulipoona hawa wengine wakubwa wakubwa ukawaelekea ukiona lift nimekialika haifai, sio? Basi hata mimi sikupi"

Bwana B akamtema.

Lesson: Usiache mbachao kwa msala upitao.

Matusi yakuom.
 

Top