Hawa wanateseka namna hii je wale walipewa migao wako wapi?

Hii picha hapa inajieleza wazi wazi kabisa. Sasa wale wabunge, viongozi wa dini na waliokuwa white house pale magogoni ambao walipokea migao ya nguvu ya mamilioni hadi mabilioni kutoka kwa hawa kupitia benk, lumbesa, sandalusi na maboksi wako wapi? Je wanakwenda hata kuwatembelea? Je kile chama kilichokuwa kinapokea misaada kutoka kwao kiko wapi? Wako wapi polisi nao waliokuwa wanachekelea misaada ya hawa? WATAPATA TABU SANA hawa lakini waliokula na kufaidi wako mitaani wanadunda na wengine ndio kwanza wanashikilia vyeo bungeni. Kwani ile listi ya waliobeba cash haitolewi?! [ATTACH=full]179360[/ATTACH]

[ATTACH=full]179357[/ATTACH]

Ukitaka uwafahamu vizuri rafiki zako waliokuzunguka basi pata shida au tatizo.

Ni hayo tu mkuu.

Dah, wanapata tabu sana.

Hali hii ya double standard ndio inatia walakini zoezi la kupambana na ufisadi.

Chenge anakula Bata mjengoni, Tibaijuka anadunda mtaani, Ngeleje alitupiga changa la macho kwa kujifanya kurudisha pesa;

Huwezi kupigania ufisadi, ukiwa na wewe ni fisadi

Kile chama chetu pendwa nao wamepiga sema wanajikausha tu.

Umemsahau Askofu Kilaini sijui yuko wapi saizi, maana huu ukimya wake sio wa kawaida

Singa amekonda shavu lote kwishaa

Sasa why msiwapeleke Mahakamani na wawo wakasotee?

Hii ufisadi iko kwa midomo tu.

inatia huruma sana yani Ruge kawa kama Burning Spear na huyo Seth ni kama wale makuani kwenye muvi ya yesu hizo ndevu

Mmmmh

Duu rugemalila kaisha

Duh, nawaonea huruma sana. Pamoja na maovu yao

yan nilikua sijui juz nikapta karb n tbc nikashtuka kumuona chenge tena kwenye kiti chao takatf sikuami nikauliza huyu ni chenge au macho yangu?, hv walimuwekaje pale nakat hakuna mbunge asiemjua, yule mzee atakua na hrz kubwa kama kichwa chake kaifukia pale mjengon, chaaa…

Mimi nalia na watendaji was serikalini waliofanikisha uchotwaji was hayo mapesa watu kama kalemani na watu waliokua ikulu na jk kwanini jiwe linafanya double standard?

Malipo ni hapa hapa duniani. Ahsante na Shikamoo Baba Mola!

Kweli mkuu, labda bado anaendelea kuzitafuna na ukimya wake huu

Madudu mengi kayafanya kuanzia kwenye mikataba feki, vijisenti hadi kwenye sandarusi, sasa ndio anakula bata kwa raha mjengoni

[ol]

[/ol]

[ul]
[li]Walioruhusu mabilioni yale yatolewe Bank Kuu na ambao walipaswa wawe wa kwanza kuanza kunyea debe kabla ya hawa wanaonyea debe leo ni;[/li][li]Rais wa nchi[/li][li]Waziri wa fedha[/li][li]Katibu mkuu wizara ya Fedha[/li][li]Gavana wa Bank kuu[/li][li]Waziri wa Nishati na Madini[/li][li]Katibu mkuu wizara ya nishati na madini[/li][li]Paymaster General[/li][li]Mwanasheria wa Wizara ya nishati na madini, hawa ndio walipaswa wawe wa kwanza kabisa kutiwa ndani maana ndio walioruhusu Fedha zile kutolewa hazina, hao akina Lugemarila mwenzake walipewa kwa idhini ya hao niliowataja hapo juu, hii vita ya kupambana na ufisadi inatia shaka sana dhamira yake kama double standard yenyewe ndio hii[/li][/ul]

Wanalipa kile walichokula
Nalog off