HEKAYA JOO

#1
Stolen FB

My group on Facebook are talking about the Kiuna's na hawajui masaibu nilipatana nayo.

Nilikuwa nafanya job airport kuexport french beans, hapo airport nikaona toto anapenda kusmile na Mimi hadharani. Mimi huyo kuomba date, nikampeleka wimpy (mshahara ilikuwa mezesha, effort) hot date, siku ingine kenchic pale karibu biashara street hapo ndio toto aliniambia vile amekubali yesu ni bwana na anatafuta mtu serious God fearing.

Jaxo saa hiyo Keg zilikuwa zangu, reggae monte Carlo sikuwa nakosa weekend.ikabidi nimskize nitaingia mambo ya kanisa juu nimeona hapo mapenzi iko moto moto.

Baada ya wiki tukaenda kanisa Thika rd, sadaka yenyewe ilikuwa color coded, bahasha ya white ni ya mathao, ya brown ilikuwa ya coins na machuani, kuna ya soo ya rwabe na ya punch. Mimi nikachukua ya white, nikaona toto amesmile yake yote, nikadunga chuani faster faster. Kidogo maombi.... Watu wanaongea na tongues, nikaanza kuongea na tongues "riririririi, I can tiriririi, I can tararara, riswa!" Toto alikuwa impressed akanishika hadi mkono juu hakuna mtu alikuwa anatingika kuniliko, lakini kuna mother Fulani alikuwa ananicheki anataka kushindana na Mimi. Punda si mbuzi watu wakaitwa mbele waombewe watolewe mapepo.
Nikaambia toto siezi enda mbele ju sina pepo. Akanishow niende tu juu ameona Mimi ni msee mpoa sana hadi anataka nilale kwake hio siku juu kwangu ilikuwa mbali....... Mimi teke teke hadi uko mbele .
Wacha kitamba irushwe watu waanguke, Mimi nimesimama the last man standing, otero. Passie ananicheki saa hiyo sikujua vile nilipigwa sweep, Mimi chini, kuamka ni problem lakini nilijitoa......Kusimama tena kuangushwa tena, saa zile nilipata mpenyo nilitoka teke si teke huko nyuma naskia passie anasema ndio hiyo pepo ilikuwa imetumwa kwa kanisa!
Mimi kwa stage kupanda 44 hadi mtaani.
Huyo toto hajawahi ongea na Mimi tena, alijua Mimi ni pepo mbaya ...
 

Abba

Busaa Catalytica
#18
Passie ananicheki saa hiyo sikujua vile nilipigwa sweep, Mimi chini, kuamka ni problem lakini nilijitoa......Kusimama tena kuangushwa tena, saa zile nilipata mpenyo nilitoka teke si teke huko nyuma naskia passie anasema ndio hiyo pepo ilikuwa imetumwa kwa kanisa!
Hii imenimalisa. Kwani ilikuwa American football?:D:D
 

Top