Hekaya yangu

2018 ilikuwa mwaka tuseme ya Baraka ama niite mwaka ya “open eye” kama Kuna maisha ingine watu huishi basi nitaishi kukumbuka 2018-2019 nikama ilikuwa Leo. Leo Sun, 28th July 2019 @ exactly 1:52am ndio niliamua kujaribu kuandika what I thought nilikuwa naishi…
2018 Jan nikaamia area code fulani inaitwa saika iko embakasi mimi uyo mpaka dandora.With the name Dandora obvious uko ni ghetto kwa mabad kids na vitu mingi zenye zimewai sifiwa “vibaya”… Pesa ikawa kokoto kwangu, Ile kidogo nilikuwa napata ndo nilikuwa najipanga nayo. Ama tuseme bora ya rent iko, ya jaba na stock ya shash apo. me nani I was well to go.
First three month was good living in dandolar mpaka vitu zikaanza kuenda U turn apo April… Kukakuja kukakuwa kugumu unapata ni rent ndo nilikuwa naeza Lipa ii ingine ya kujibamba ilikuwa night mare but tushukuru God ju nilikuwa nishaapata maaref mtaa saa unapata kukisota ivo wananiinua kimwanaume.
Stivo akakuja akaama hio place ju ya Vita ya vijana na makarao (io nikumaanisha story ya shash nilikuwa nipunguze ju kwa rende mimi na yeye ndo tulikuwa tunaiva) Tukabaki mi na Ben who loved Jaba kashit!
Every day was a weekend na tena si ati kanashikia mbali ju club ilikuwa down stair baze ya jaba haungeenda steps kumi kutoka kwa gate ya Goro nilikuwa naishii. After club usiku kalikuwa kanashikia kejani tu. Bora mayeng wakuwe present, Jaba, shash, tools, ngoma, na tei io ingine nikuwachia sir Jah atufikishe asubui… Mara mob ningeechangamkia job afternoon same applies to Ben.
My Girl never liked dandora kwaivyo alinipressure nitafte nyumba area code ingine of which nilijikakamua Ata ka sikuwa poa mfuko nikajipata man cave area code ya mowlem (niwachekeshe keja yenyewe alikanyaga twice pekeake) after apo story yangu na yeye ikadissolve ivo life ikawa worse than the way it was nikiwa dandora. Rent ilikuwa cheap na kuzidisha kuipata ilikuwa sheda. job yangu ikaanguka yani tuseme shetani akamua kukuja na mashida plus na family yote ya mashida kejani kila siku mashida iliakikisha zimeimba wamnyonyez walambeza. Nawaambia apo ndo nilianza kulambwa na mashida… Zile sufuria nilikuwa napika nyama nazo nikaanza kupika uji. Na kumbuka Kuna siku Ata hio Unga ya uji nilikosa nikaamua kukul tomato zilikuwa apo kwa shelve na chumvi.
Left RIGHT KO za mashida mpaka nikaona ama mi ndo niliachwa na Mungu na sijui. Kwaivyo after seeking help huku na pale Kuna neighbor door number 2 akaniambia niaje, solution ni yesu niwachane na solution ya fombe na miraaa. Ukweli nilipunguza fombe nikaingia kwa injili, sijui mbona ukiingia kwa injili lazma Ile squad ulikuwa nayo ikutoke hahaha. Your boy sokomtu akabaki ivo bila rafiki. Nikachapa hustle online ya marketing yenye every weekend ningepata 500 Bob nijipange 250 airtime nahio ingine nikusave,chakula ilikuwa kutime jirani aunguze kitungu alafu unaenda kuwatch news kwake. (by the way haikukawia jirani akagundua tactic ya sapa yangu akauza TV)
To cut the long story short nilikuja nikalemewa na maisha nikarudi ocha where niliuza ndama ya mzee nikanunua mbegu na mbolea nikaanza Ukulima wa ndizi. Ndizi ikafanya vizuri mzee akapata ndama ingine na mimi nikarudi Jiji kupambana na maisha ka wengine. Maisha haijakuwa nyweee ivo lakini kwa sahi naeza Sema come rain come sunshine hakuna kitu inaeza nifanya nililie kwa Choo hii Nairobi. About the girl ni another story ya siku ingine na venye nilikuja kugundua kumbe kifudaa alinitoka ju ya my best friend mwenye alikuwa na mandevu kunishinda na juu alikuwa anaishi kwa one bedroom mi nikiwa kwa single house

hahhaha wow malizia hekaya boss:D:D:D

hujawai enda kununulia huyo jirani kanyama ukimkumbusha hii maneno.

Vile watu husema Nairobi Ni shamba ya mawe hua hawadanganyi. Kama Hauna biz ama job utalala njaa ama ufungiwe mlango ya keja. Watu wengi don’t realize huku nai Kuna pesa. Kama Hauna job Kuna places mob Zina recruit on a weekly basis. Biz mingi za hoteli, bar, security, sales, factory, Sacco ya mathree ziko na interview kila siku. Shida ya mayout Ni kuchagua job ati mabeshte ama family watanicheki vibaya wakijua unafanya job ya watchi G4S. Lakini Hawa mayout Hawa realise G4S inasort salo ya 20K. Hii Doo ita kusort vipoa ujipange. Mimi husema Kama haujipangi kimaisha, maisha itakupanga.

Ukulima was ndizi?
And in less than a year you already back on your feet?
Apparently your mungu performed a miracle…

Acha niiweke ivi, [ATTACH]250687[/ATTACH]Ukulima na mpango…

Punguza bangi, naona uko na hekaya mingi angusha kadhaa Omwami.

you stole my thoughts.

Hapo sawa but usiwai taja tena hio ujinga ya wamlambez kwa hiki kijiji