Hii forums ina uhuru mkubwa sana!

Ukitembelea nzuzi mbalimbali humu Kenyatalk na kuona zinavyowasilishwa utaona kwamba hawa jamaa wana uhuru mkubwa sana wa kujieleza. Wakati mwingine Lugha zinazotumiwa na wenyeji wa Kenyatalk hukuacha mtu umeasama mdomo. Kuna baadhi ya thread humu zingekuwa kule nyumbani tayari wenyewe wangekuwa wako jela.

Nilichogundua hoja hazifutwi bali hujibiwa kwa hoja ama wakati mwingine kwa mitusi ya nguoni. Pekee ninachojiuliza kama matumizi ya matusi kwenye kujibu hoja inatokana na uchache wa misamiati ya Lugha waliyonayo wakenya ama ni kutokana na tabia walizo nazo.

Yanini sasa kufananisha nchi mbili tofauti kwa mnadhili mmoja? Hukupaswa kutambua ya kuwa kunde ni kunde na maharage ni maharage? Yakufaa nini kutaka ngano kuwa kama mahindi?

Wakati mwingine kuchanganya vitu hufanya vitu kuwa bora zaidi. Jee kugundua kwamba ngano na mahindi ni tofauti siyo hatua kuelekea kwenye ufahamu bora zaidi kuhusu vitu hivyo!?

Jamaa ndio jadi yao

Najifunza mengi sana humu kutoka kwa hawa jamaa.

Kwanini sasa wataka kuchanganya maji na mafuta? Huoni havikuweza kukaa pamoja hata kale?

Nahis hawaelewi matusi hayo ni mazito kiasi gani kwa kiswahili.

Wahuni tu hao, wanafanya makusudi kwa cover ya eti hawajui Kiswahili.

Hii itakua mbaya zaidi kwa Serikali yetu maana haina moderation strict kama JF

Na wewe kuna baadhi ya comments zako naona unaandika kiswahili cha huku mafichoni tulipo, hahahahahahahahah

Huyu na @Dave Mtzd (Nyani Ngabu?) washalowea kabisa!!

Hivi Dave mtzd ndiyo Nyani Ngabu, mbona amekuwa mtu cool sana!!!.

May be, may be not!!

Si pia nyie mna matusi
Kama vile:-
1.boya
2.kilaza
3.pia mna penda kusema"toa upumbavu wako hapa"
Matusi ni matusi

Sisi tunapenda kutumia tafsida. Badala ya kusema fulani ni mshenzi, sisi husema fulani si mstaarabu!

Hivi hauoni huo ni una fiki wa ki aina.una mtusi mtu eti kwa ustaarabu ndio badae usipate lawama. unajaribu bado kuonekana kama mtu mzuri lakini cha msingi nikua ume mdhalilisha na jama atakua kesha kasirika.

Kenya hakuna cha kuficha,kama wewe mkora bora tukuite mkora na hilo liishie hapo.

Kila lugha ina kanuni zake, tafsida si unafiki bali ndiyo matumizi yenyewe ya Lugha ya kiswahili. Kwa mfano si sawa kumwambia mtu mzima wewe ni mshenzi lakini ni rahisi kumwambia kwamba wewe si mstaarabu na ivo maana yake mtu ambaye si mstaarabu ni mshenzi!

Swali langu ni hili…mbona usi mwite tu yule jama mshenzi?
Si ni bora mambo ya wekwe bayana ili mradi yawe ni kweli??

synthesis of opposites begets higher truth.