HII INATOKEA TANZANIA TU!

#1
14484961_1748187422103308_967198746446976567_n.jpg
Ni Tanzania tu ambapo mdada anajua kabisa tarehe ya kuvalishwa pete ya uchumba (engagement), anashona nguo, na anakwenda saluni, halafu mwanaume mchumbiaji anapokuja na shamrashamra zote siku ya tukio, eti akitoa pete kumvalisha mdada huyo anajifanya kushangaa sana (SURPRISED)! Kuna mmoja alizimia kabisa wakatI ni yeye ndiye aliyetafuta mpaka sonara!
TUNAISHI KWA KUIGIZA!...
 

Smart911

Village Elder
#13
Wanawake wengi wa siku hizi ni kheri ajue siku ya kumvalisha pete kuliko kumfanyia surprise...

Unaweza mfanyia surprise, ukaambiwa hapana, kwanza tuma washenga kwetu, wajuane na wazazi, wakubaliane , wajibiwe alafu ndiyo urudi kunifanyia suprise ya pete ya uchumba sasa...


Cc: @Mahondaw
 
#19
Hahahaaa. Wana Simba mnasemaga "this is Simba" na huku ukimbizini hii tunasema "this is KenyaTalk"

Na maisha mengine yanaendelea hapo yaani hakuna cha Mods kufuta Post wala kuedit Post. Teh teh
Mods wa Kenya tungekua nao kule JF basi kusingekua na haja ya kua na Jukwaa La Wakubwa, kila kitu kingekua hadharani maana wabongo ukiwaachia kila kiungo cha mwili kitaitwa kwa jina lake
 

Hajar

Village Elder
#20
Hahahaaa. Kwa hilo la kuvishana pete waeza kuta mdada ndio amelazimishia na mwanaume ye hakuwa tayari na ndio sababu yanatokea yakutokea watu kujinunulia pete wenyewe.

Hapa labda useme wanawake ndio tuendane na mwendo wao wa Kobe yaani mpaka pale wakiona sasa huu ndio muda wa surprise japokuwa kwa mbaali walio wengi wanaachwaga kwenye mataa. Yaani wanatumiwa mpaka basi na mwisho wa siku anasurprisiwa mwingine. Teh teh.

Hahahaaa ndivyo tulivyo mkuu, tatizo lipo kwa wanaume kwa nini msifanye suprise hadi mtutangazie
 

Top