HISTORIA YA MWANZILISHI WA FACEBOOK MARK ZUCKERBERG

Kuzaliwa: 14/05/1984
Mahali: New York Marekani
Baba: Daktari (Mganga) wa vichaa
Mama: Daktari (Mganga) wa meno

Ana asili ya wayahudi (Jews/ Hebrews) wa Israeli lakini yeye mwenyewe hana dini na haamini kuwa kuna Mungu.
Facebook ilianzishwa mwaka 2004 na Mark Zuckerberg na wenzie wanne akina Dustin Moskovitz, Eduardo Severin, Chris Hughes, na Yuri Milner wakiwa wanasoma chuo kikuu cha Harvard, Marekani. Chuo hiki wamepita nguli wengine wengi kama akina William Gates(Bill Gates) n.k. Sasa wote waliacha chuo kikuu cha Havard walipokuwa wakisoma masomo ya masuala ya teknolojia ya mawasiliano na kuwazidi akili wanafunzi wenzao na maprofesa. Zuckerberg alikuwa kiboko tangu siku za awali masomoni hapo, alikuwa akibuni mitandao ya aina mbali mbali kwa ajili ya faida ya wanafunzi wote.

Hata Facebook yenyewe alianza kuitengeneza yeye kwa ajili ya mawasiliano ya wanachuo wenzake wa Havard. Lakini siku chache baadaye, mtandao wa chuo ulizidiwa nguvu kwa matumizi yake na ndipo ikafahamika kuwa watu wengi wameupenda. Ndipo Zuckerberg akawaita hao wenzake wanne na kuamua kuwa mtandao huo utumiwe na wanafunzi wa vyuo vikuu vyote vya jirani na chao cha Havard kufanya mawasiliano miongoni mwao.

Baada ya kubaini kuwa Facebook ambayo wakati huo ikiitwa Facemash, ulikuwa mtandao uliopendwa sana, vijana hao wakaamua kuacha masomo na kuanzisha kampuni iliyoufanya mtandao huo kuwa maarufu sana kama tunavyoona sasa. Na rafiki zake na Zuckerberg wote wameingia katika orodha ya watu matajiri zaidi dunianiingawa yeye amewazidi kwa kuwa anamiliki hisa nyingi zaidi. Tangu akiwa mdogo alionesha kuwa genius, katika masomo yake ya shule ya msingi, bilionea huyu alikuwa akishinda tuzo katika masomo ya Sayansi na Hisabati mara kwa mara.

Wakati akiingia sekondari (shule ya upili) Zuckerberg alitakiwa kuandika lugha nyingine mbali na kiingereza ambazo angeweza kuzizungumza kwa ufasaha. Aliandika 1. Kifaransa 2.Kiyahudi 3. Kilatini 4. Kigiriki jambo lililowashangaza wengi. Zuckerberg ni mpenzi mkubwa wa simulizi za kale za Kigiriki na kwa vile nyingi zilikuwa zimeandikwa katika lugha ya Kilatini aliamua kujifunza lugha hiyo (lugha hii inakufa kwa kuwa inakosa watumiaji) ili aweze kuzisoma moja kwa moja bila ya kutafsiriwa kiingereza.

Wanafunzi waliosoma naye wanadai kuwa enzi zake chuoni alikuwa akisoma sana vitabu vya kigiriki kiasi kwamba alikuwa na uwezo wa kusoma sura nzima ya kitabu cha ILIAD kutoka kutoka kichwani kwake. Kwa kuonesha kwamba ana vipaji lukuki, Zuckerberg alijifunza lugha ya kichina kipindi anamchumbia PRISCILLA CHAN ambaye ni mkewe na wana mtoto mmoja wa kike aitwaye MAX pia mbwa aitwaye Beast mwenye ukurasa wake mwenyewe wa Facebook!. Mkewe ana asili ya Uchina na bilionea huyo alidhani kuwa ni muhimu kwake kujifunza lugha hiyo kwa vile sasa Uchina ina nguvu kubwa za kiuchumi. Pia Zuckerberg aliweza kuisajili Facebook kwenye soko la Hisa la Wall Street.

Alipokuwa akiuzungumzia mtandao wake wa Facebook, Zuckerbeg alidai kuwa wakati akiuanzisha lengo lake halikuwa kutajirika isipokuwa kurahisisha binadamu kufahamiana na kubadilishana mawazo. “Wakati nikiwa mwanafunzi na hata katika hatua za awali za Facebook makampuni mengi makubwa yalinifuata kwa lengo la kutaka niyauzie kampuni (Kama Elon Musk alivyoiuza Paypal na kuanzisha Tesla(Kampuni ya magari ya umeme) na kampuni nyingine kadhaa) na wenyewe waumiliki mtandao huo lakini nilikataa”. " Kama shida ingekuwa ni fedha ningekuwa nimeuza zamani mtandao huu’‘. "Fedha si kila kitu katika maisha na bado ndoto zangu kuhusu Facebook hazijatimia’'.

Kitu ambacho wengi hawafahamu kuhusu Zuckerberg ni kwamba ana tatizo la kutoona vizuri rangi yoyote ambayo ndani yake ina mchanganyiko wa rangi nyekundu na kijani. Hii ndiyo sababu rangi ya mtandao wa Facebook ni bluu kwa kuwa hiyo ndiyo rangi anayoiona vizuri kuliko rangi zote zingine. Zuckerberg ni mtoaji mzuri wa misaada ya kijamii na wana mfuko wao unaitwa CHAN ZUCKERBERG INITIATIVE https://www.chanzuckerberg.com/ kwa ajili kufanya utafiti ili kuweza kutibu magonjwa mbali mbali kwa watoto.

NIKIRUDI NTAJARIBU KUELEZEA ALIVYOVUNJA FARAGHA ZA WATUMIAJI KUPITIA CAMBRIDGE ANALYTICA

https://www.youtube.com/watch?v=66uO0qNL5qI

Don’t please, thank you. meffi

Effect za jamiiForum closure…

Musa akifikiria awekelee lusimbo agawanyishe maji.

@Immortan Joe why not unanipangia cha kupost humu www.kenyatalk.com?

@That Guy Thrill wala am not a new member here.

[ATTACH=full]175453[/ATTACH]

Sawaa