Hivi Mambo Ndio Yamefikia Hivi?

Mwendo wa kuviziana!
Mmiliki wa mgahawa wa bunge Bw.Daniel Lamba amepigwa faini ya Sh.300,000/= baada ya kukutwa na kilo tatu za samaki aina ya sato (samaki 7) ambao hawajafikia urefu unaostahili kuvuliwa. Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw.John Mapelele amesema baada ya kupimwa (kwa rula) samaki hao wamedhibishwa ni chini ya sentimita 25 ambao hawaruhusiwi kuvuliwa kisheria. Mmiliki wa mgahawa huo amesema amenunua samaki 100 leo asubuhi, na hakujua kama alichanganyiwa samaki ambao hawajafikia urefu unaostahili kuvuliwa. Wizara imesema inamsaka msambazaji aliyemuuzia Lamba samaki hao ili kubaini mtandao wake.

[ATTACH]177526[/ATTACH]

Wao wanawezakujisifu kuwa wamefanya la maana sana!

Kweli mkuu inashangaza sana

Huyo mkaguaji ni mchafu sana.
Na mikono yake katoka chooni ati anapima sanaki.
Wakiwa wadogo ndo hawaliwi?

Dunia hii maajabu hayaishi!

duh,nimecheka yangu yotee

Tz wanakatazwa upande wa Rwanda, Kenya,Uganda na Burundi wanaliwa bila kujali size

Ndipo utapopima Tz tunaainagani ya uongozi!

hata mafuta na bidhaa atunze risiti.

pale wizara inapokosa kazi za kufanya (labda kwa kutokana na uhaba wa fedha) haya ndio matokeo yake, inachekesha na kusikitisha kwa wakati mmoja. huwezi kutembea na rula nchi nzima kupima samaki migahawani, samaki (sato) wanakovuliwa kunafahamika hivyo ni rahisi kutoa elimu na kudhiti uvuvi haramu huko , hayo mengine ni MAIGIZO

wai!

Jamani naomba kujua, Sato wa ziwa Victoria wanavuliwa Uganda na Kenya pia. Jee huko nako sharia ya kupima kwa rula inatumika? au Sato wanaovuliwa Tanzania wana alama ya bendera ya taifa kujulikana kuwa hao ni wa huku kwetu?

Hivi Samaki akipikwa anabaki na ukubwa wake ule ule au mimi ndio sielewi?

!
!
Very Reactive. Pumbavu Kabisa. Wako Bize Kutibu Dalili Huku Ugonjwa Ukiendelea Kutumaliza.

too much is harmful

Yaani kwenye kilo mia, pisi tatu mtu unapigwa faini laki tatu… halafu mkamataji waziri mwenye dhamana…hii zaidi ya hatari.

Kwani samaki wote wanatoka ziwani? Sasa hv watu wengi wana mabwawa yao binafsi hivyo mtu anawauza muda na ukubwa wowote apendao. Hapo watu wenye akili hizo wanakuambia wanaelekea kwenye nchi ya viwanda!!

Mzee @Lubaragazi A1 nipo huku

wajukuu zako watakula nn??

mkuu were u banned???

[QUOTE=“ROBERTO 20, post: 1677990, member: 37034”]
mkuu were u banned???
[/QUOTE

Hapana hyo ni avatar[/QUOTE]