Mkuu,Hapo ndipo wachungaji wanapowapotosha wafuasi wao,naweza kukwambia kuwa Yesu hakuwahi kujenga kanisa,hamna hata sehemu moja katika biblia Yesu amesema kuwa yale anayoyahubiri yanaitwa dini ya Kikiristo,…Hiyo mistari ya biblia matayo Matayo 15:22-24, niliyokuweka iko wazi kabisa,Kuwa yeye Yesu alikataa kumtibu mtoto wa yule mama kwasababu yule mama na mwanawe walikuwa sio wayahudi,haina haja ya kutafsiriwa na Mchungaji ili uifahamu
Wana wa Isaeli waliopotea ni wale wayahudi waliokuwa hawafati mafunzo ya kitabu cha “Taurati”,kulikuwa hakuna Ukiristo wakati huo Yesu hakuhubiri “Ukiristo”,Yesu aliendeleza mafunzo ya kitabu cha Taurati,kitabu cha Musa(Moses)…
Kuna kisa chengine katika biblia Yesu aliwambia wanafunzi wake 12 kuwa wasiende kuhubiri kwenye nyumba ya mtu yeyeyote sipokuwa nyumba za Wayahudi,kwanza yeye mwenyewe alikataa kuwatibu watu walikuwa sio Wayahudi halafu aliwaamrisha wanafunzi wake wafanye hivyo hiyvo….,kama ilivyoelezwa kwenye Matayo 10:1-7
[SIZE=5]Matayo 10:1-7 : Bibilia Takatifu [/SIZE]
Ndipo Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa mamlaka ya kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. 2 Majina ya hao wanafunzi kumi na wawili ni haya: 3 wa kwanza, Simon, ambaye aliitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo, mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake; Filipo na Bartholomayo; Tomaso na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; 4 Simoni Mkanaani; na Yuda Iskariote ambaye baadaye alimsaliti Yesu. 5 Yesu aliwatuma hawa kumi na wawili(12), akawaagiza, “Msiende kwa watu wa mataifa wala msiingie mji wo wote wa Wasamaria. 6 Bali waendeeni kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. 7 Na mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia
Mkuu hii mistari haina haja ya kutafuta mchungaji akutafsirie,labda uwe hujui Kiswahili,Wana wa Israel imekusudiwa Wayahudi,kwa kiarabu wanaitwa “Bani Israel”,Wana wa Israel sio Wakristo kama unavyosema wewe,usipotoshe maana na ujumbe aliokuja nao Yesu kwa binadamu