Huku tutajua mengi kuliko TZ

Mfano, hii kitu Mello asingelikubali kuiweka hadharani. see attachment

Aise

Kumbe bora tubakie huku huku Ukimbizini! Haya wale wajinga wa kutetea kila uozo wa CCM kujeni huku!!

Patamu…

Jambo ninalojiuliza ni kwa nini jambo dogo kama hilo nakala imekwenda mpaka wa Rais?

haya ya tano, inasema documents zinaonesha ni mzigo binafsi wa paul makonda na sio ofisi ya mkuu wa mkoa. HSC??

Ujue vitu vingi unavyoona wewe vya kawaida Raisi anaingilia…ndio maana viongozi wa ngazi za chini wanashindwa kujiamini mbele yake.

Makonda alitaka kukwepa kodi kwa kutumia kivuli cha Mkuu wa mkoa…Mzigo ameagizwa kwa jina lake binafsi halafu anaomba utolewe kwa jina la mkuu wa mkoa.

Kwa kweli jinsi tunavyoendesha mambo yetu wakati mwingine inatushangaza hata sisi wenyewe. Hapa ndipo Ofisi ya Mwendesha mashitaka wa Serikali ilitakiwa kuanzisha uchunguzi wa jambo hili. Hao watanzania walioko Marekani ni kina nani?

Halafu ni kwa nini Mpango anamshauri Makonda abadili jina la anayepokea mzigo?

Ingekuwa tunajali uwajibikaji bila upendeleo sasa hivi Makonda ilibidi afanyiwe uchunguzi wa kina.

Kwa kuanza ndani ya nchi hadi nje ya nchi, lakini waziri wa fedha anajibu kirahisi rahisi tu tena kwa kumsaidia mkwepa kodi…

Hii nchi yetu inatia aibu sana.

Labda anaogopwa! Maana mtirirko wa nakala ni dalili kwamba Mpango aliingiwa na woga mkubwa sana!

Mzigo utaagizwaje kwa jina binafsi alafu atake utolewe kwa jina la ofisi?

Unajua utaratibu wa public Procurement act?

Hilo swali nadhani ungemuuliza Makonda.!

Ndicho ninachokishangaa hata mimi. Barua inayoandikwa na waziri halafu kopi anapewa katibu mkuu wa wizara hiyo hiyo! Au hakuna mawasiliano ya ndani kati ya waziri na katibu mkuu wake?

Hapana inavoonekana Mpango alikuwa anaweka ushahidi asije akarukwa mbele ya safari akatumbuliwa bila ya sababu.

Kaona bora kujihami mapema.!

Ukiangalia hii issue vizuri, Waziri Mpango amewa cc wote hao ili kuweka record sahihi maana anajua fika anadeal na vichaa wawili…
RC na Baba yake.

hujui masifa ya jamaa

Kajisemea Zitto: nchi inaongozwa na washamba. Maana hata taratibu za kawaida hazifuatwi. Wasichojua ni kuwa kutofuata sheria kunasababisha watendaji washindwe kutimiza majukumu yao - maana mtu huwezi kujua nini kitatokea ukiamua jambo.

Kwenye ilani yao: Wasichana watakaopata mimba wataruhusiwa kurudi shule
Mkurugenzi wa Sekondari (na baadae waziri wa elimu): Tumeandaa policy ya kuruhusu wanafunzi kurudi shule baada ya kujifungua
Makamu wa Rais: Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha kuwa wasichana hawanyimwa elimu kutokana na kupewa mimba
Magufuli: Nisomeshe wazazi?? Yayaaa!

Halafu bado kuna mtu alishangilia kuanzia mwanzo hadi mwisho!

[FONT=tahoma]Duh…balaa kubwa aliyakana makontena yake mchana kweupe kumbe alishaomba msahama wa kodi na mizigo imeingizwa kwa jina lake binafsi sio la ofisi yake.[/FONT]