Huu Ujumbe uwafikie Tanzania Revenue Authority (TRA)

Hivi zile Tsh 40,000 tunazolipia pindi tuna renew leseni za udereva huwa mnapeleka wapi??? Haiwezekani mtu umelipia hela toka mwezi march mwanzoni ili upate leseni yako lakini hadi mwisho wa mwezi huu wa sita eti leseni haijatoka!! Hiki si ni kituko na aibu?? Kama mmeshindwa si mtangaze tenda watu wachukue tenda kuliko kufanya vitu vya aibu?? Maana kila siku ukienda kuulizia kama leseni yako imetoka utaambiwa Material yameisha hii ni aibu sana, Je zile hela tunazolipia huwa mnafanyia kazi gani??
Mbona haya mambo zamani hayakuwepo???

Mimi nategemea nikapewe mafunzo ili niwe dereva wa Uber & Taxify, ila kinachokatisha tamaa na kuvunja moyo nikipeleka risiti yangu niliyopata baada ya ku renew leseni ya udereva naambiwa hawapokei hizo risiti wao wanataka leseni iliyo valid, nikienda kuulizia TRA leseni yangu vipi haijatoka?? Naambiwa material yameisha, Je ni vijana wangapi kama mimi wanapitia hii shida?? Mnataka tukakabe?? Maana nyie ndio mnaweka uzibe, Tukiongea mitandaoni uzembe na upuuzi kama huu kwenye mitandao ya kijamii mnaifungia!! Mnataka shida zetu tukawasilishe wapi??? Hawa TRA wanaosema wanakusanya Trillioni kwa mwezi wanashindwa kweli kununua material kwa miezi 4 kweli??? Inauma sana.

NB: Kwa anaejua kama kuna njia naweza tumia ili nisajiliwe kuwa dereva wa Uber kwa kutumia risiti yangu niliyopewa naombeni mnisaidie kwa ushauri maana sijui nitumie njia gani nimesubiri miezi minne bila mafanikio yoyote maana kwa sasa sina chanzo cha kujipatia kipato cha uhakika.

Duuh

pole sana mkuu. Serikali yetu ni kwamishaji sana. Ukienda kufungua kampuni wanasema wanataka kitambulisho cha uraia. Ukienda NIDA kupata kitambulisho hata miezi 7 inapita.

Yaani ni kituko!!wanataka mapato yote yaingie kwenye kapu moja ili wajisifie kuziona zimejaa !!kimbembe ni pale wanapoambiwa sasa mmeshaziona zirudisheni kwa wenyewe(halimashauri na taasisi )ndio sarakasi zinaanza!!kwani wanadhani makusanyo yote ni faida tupu hawajui kutoa gharama za uzalishaji!!!wanaona kutoa tena kununua materials ya leseni ni hasara!!!refer sakata la korosho wamepokea bilioni 210,wanarudisha eti bilioni 10!!!..wa ajabu ambaye hajawahi kutokea!!!mapato ya leseni yanaenda kutoa msaada kwa mgonjwa!!!

hela hakuna za kununua material mkuu… kwani hujui mapato yote yako chin ya bw mmoja ambaye hatoi had aamue…!

Tunakusanya kwanza. Mtuvumilie. Haaaaahaaaaaa.

Hii NIDA ndio takataka kabisa.

Hapo kwenye kutangaza tenda umeongea la maaa mkuu kwasababu serikali inakua kama bongo movie tu unakuta vitu vyote anataka kufanya mtu moja wakaki uwezo wa kuvimudu haupo…

Hii inapelekea ubovu wa kazi ata muda pia hauzingatiwi kama unavyosema hapo juu

Mkuu leseni yako imeshatoka siku nyingi sana sema tatizo unaonekana una mkono mzito kidogo.
Hii nchi sasa kila kitu ni pesa, toa pesa then utapata leseni dakika hyohyo hzo za materials hamna ni porojo tu

Pole sana, pesa inajenga reli na kununua ndege kwanza.

Aisee!..

Umenena ukweli…wiki 2 tu unapata leseni …mwache asubiri mpaka inakaribia kuisha ndio apewe…

Amini Mkuu… ukiwa na mkono mzito hii nchi utasafa sana. Hapo wanamsubiri tu siku ajiongeze then atashangaa mtu anavuta droo anamtolea leseni yake.

Sidhani kama ni kweli mkuu nimejaribu njia zote serikali yetu naijua hadi hao wa kuwapoza nao wanalalamika kupiga hizo deal wanasema material yameisha.

Hamna mkuu inaonekana ni kweli material yameisha, nimejaribu kutokuwa na mkono wa birika ila wapi wanasema material yameisha.

Hakuna leseni mpaka mwezi wa nane,kampuni inayodai huko norway haijalipwa

Basi soon zinakuja Electronic License, coz hata kwenye Passport walifanya the same, delaying for four months

Eeh yani bora tenda itangazwe ipewe kampuni nyingine kuliko kutaka kufanya kila kitu wao mwisho wa siku matokeo ndio haya leseni inachukua miezi 4 kutoka, hii si ni aibu sana kwa spidi hii bado tuna safari ndefu sana, halafu me nashangaa mbona zamani hii kitu haikuwepo???

Kama ni kweli basi inaelekea hela tunazotoa huwa zinafanyiwa mambo mengine mbona hii SIRIKALI kituko aise.

Sorry Boss