Jamani mwenye muswada wa vyama vya siasa unaobishaniwa atuwekee hapa! Hebu ona majibu ya msajiliQQQQ!!!!!!!!

msajili wa Vyama Vya Siasa amevitaka vyama vilivyoitisha mkutano wa kuupinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa kuacha propaganda za kupotosha muswada huo kwa sababu hatua zote za mchakato wa maboresho walishirikishwa. Ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kufanyika mkutano wa vyama 15 vya siasa ambavyo pamoja na mambo mengine, vilitangaza kuupinga hadharani Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa vikidai unatengeneza kaburi la vyama vya siasa na demokrasia nchini.
Akijibu hoja za viongozi wa vyama hivyo kwenye mahojiano yaliyofanyika Dar es Salaam jana, Msajili Msaidizi wa vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alidai kilichosemwa na viongozi hao ni upotoshaji na kutengeneza propaganda za uongo. Alisema lengo la serikali katika sheria mpya ni kuhakikisha vyama vya siasa nchini vinapata sheria bora inayokwenda na wakati ambayo itatoa nafuu kwa vyama vya siasa kuendesha shughuli zao kwa uhuru na kwa mujibu wa katiba za vyama vyao.
Alisema hakuna kipengele ambacho kinampa mamlaka msajili kuingilia uamuzi wa ndani ya vyama vya siasa.
Kwa mujibu wa Msajili, ameshangazwa kusikia marekebisho hayo yanakwenda kuua au kukandamiza vyama vya siasa wakati siyo kweli kwa sababu vyama hivyo vilitoa maoni yao wakati wa mchakato wa maoni mpaka hatua ilipofikia.
“Sasa kama wanaona muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa unakwenda kuua au kuvikandamiza vyama kwa nini walitoa maoni yao?.

Alisema kilichofanyika kwenye muswada huo ni maboresho ya kawaida ambayo vyama na serikali wamekuwa wakifanya kwenye sheria au katiba zao kuhakikisha
wanapata sheria bora.

Miye sasa naelewa kuwa kuna watu uzao wao ni shetani! Kama kweli kuna upotoshaji hapa!!!

huyu msajili ubongo/akili uko kwenye anus! Anasemaje?

Mambo wanayafanya wenyewe alafu wanakuja kujipinga na kubishana…

Cc: @Mahondaw