JE, KWANINI TUNAFOKA?

Mwalimu Mbobezi wa Saikolojia akiwa anafundisha kuhusu mahusiano, aliwauliza wanafunzi wake: “Kwanini tunafokea na kukaripia tunapokuwa tumekasirika? Kwanini watu wanafokeana na kukaripiana kwa sauti kubwa?”

Wanafunzi wakafikiri kwa muda, mmoja akasema, “ni kwa sababu tunakuwa tumepoteza utulivu wa nafsi na hasira inakuwa juu sana”. Lakini Mwalimu akauliza tena, “sasa kwanini upige kelele kwa nguvu wakati yupo hapo jirani yako na hayuko mbali?”

“Je haiwezekani kuongea naye kwa utaratibu na kwa sauti ya chini? Kwanini unapiga kelele kwa mtu akiwa amekuudhi?” Wanafunzi waliendelea kumjibu lakini hakuna hata mmoja aliyetoa jibu la kumridhisha Mwalimu.

Baadaye, Mwalimu akawaelezea hivi: “Pale watu wawili wanapokuwa na hasira kila mmoja na mwenziwe, kisaikolojia kunakuwa na umbali wa mioyo yao. Kuweza ku-cover huo umbali, lazima wafokeane kwa nguvu na kwa sauti ya juu ili waweze kusikilizana. Jinsi wanavyokuwa wanazidi kupata hasira na ndiyo jinsi watazidi kupaza sauti zao kwa sababu na umbali wa mioyo yao unaongezeka.”

Baada ya hilo jibu Mwalimu akauliza tena: “Inatokea nini pale watu wawili wanavyopendana?” – akajijibu kwa kusema kwamba “hawawezi kukaripiana ila wataongea taratibu na kwa lugha laini, kwanini? Ni kwa sababu kisaikolojia mioyo yao ipo karibu kabisa.

“Umbali wa mioyo yao ni ndogo mno.” Mwalimu akaendelea: “Pale watakavyozidi kupendana zaidi, nini kinatokea? Hawataongea, watanong’ona tu hata kama wakiongea kwenye simu, na watazidi kuwa karibu mno katika mapenzi yao. Na mwishowe hawatahitaji kunong’ona tena, bali wataangaliana tu na basi kila mmoja atapata ujumbe kutoka kwa mwenzake hasa kwenye tendo la ndoa.

Hivyo basi, mtambue kwamba pale mnapogombana na wapenzi wenu mnatengeneza kaumbali fulani kati ya mioyo yenu na ya wapenzi wenu. Na ndivyo taratibu mnavyoua mahusiano yenu. Kukwaruzana kwenye mahusiano hakukosekani, ila ni vema mkasuluhishana mapema na kurudi katika hali ya kawaida.”

Mungu abariki mahusiano yenu, akawaondolee kila aina ya kikwazo, mkaishi kwa furaha na upendo huku mkizikumbuka zile nyakati za mwanzo wakati mapenzi yenu yakianza!

Si vibaya tukisema ‘AMEN!’…

Ameni

Amen

Amen inamaaana gani

Its true,with no doubt…

Na iwe hivyo.

Amen

“Baada ya hilo jibu Mwalimu akauliza tena: “Inatokea nini pale watu wawili wanavyopendana?” – akajijibu kwa kusema kwamba “hawawezi kukaripiana ila wataongea taratibu na kwa lugha laini, kwanini? Ni kwa sababu kisaikolojia mioyo yao ipo karibu kabisa.” KUNA MWANA-JF NIMEUSOGELEA MOYO WAKE LKN HATA HAJALI!

kumbe

Hahahahaaa…

Hujamfungukia tu, asa atajuaje kama moyo wako umemkaribia