JE, UNAJUA KWANINI HUFANIKIWI?

Hufanikiwi kwa sababu una mizigo mingi isiyo ya lazima wala faida ambayo umeibeba:

  1. Umejipa jukumu la kuwa “mpelelezi” wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.

  2. Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.

  3. Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako wa karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!

  4. Umeweka mbele zaidi “watu watanichukuliaje” kuliko kuangalia maisha yako. Watu ndio wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.

  5. Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna. Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.

  6. Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii. Huna siri hata moja! Hivyo, unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema “umefulia”

  7. Kila aliyefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.

  8. Upo sahihi kila siku (you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndiyo sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia “hapa umekosea” kwa sababu ya ujuaji wako (much know).

  9. Hujifunzi maarifa mapya. Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni “Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe” Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi “life skills” wala ujuzi mwingine.

  10. Unazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako kujiunga na bando.

Hebu ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli unahitaji kusonga mbele…

Umejiuliza kwa nini huu uzi hauna wachangiaji?

Bado sijajiuliza, labda uniambie kwanini imekuwa hivyo!..

Hauko katika mfumo wa “ngono”

Soma tena between the lines ile post yako utagundua…

Haahahaa…

Kazi ipo.

:D:DMule mule, jiwe gizani

Mkuu leo naona umeamua kutoa nasaha za wahenga. Umepiga pazuri kwani utakua umegusa kundi kubwa la watu. Bigup brother.

Namba tatu (3) umerusha jiweni gizani limenipata: kele uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii nakufwaaaaa.

Ni kweli kabisa ila nivigumu mtu kuyaepuka yote hayo uliyoyaorodhesha
Hata waliofanikiwa bado wana baadhi ya mambo kama hayo

“Hata waliofanikiwa bado wana baadhi ya mambo kama hayo”
Ni Bora Awe amefanikiwa, kwa vijitabia hivyo kujifananisha nae ili hali mafanikio hafanani nae ni Kujifariji moja wapo.

Kuna ukweli apa

au nikupe mifano halisi ndio utaamini

Jf yaanza kurudi taratibu…! Soco soco

Sawa mkuu nmeongeza elimu bt no. 10 inanisaidia siiachi ng’o.

Ha ha ha haaaa…

Bado sijaelewa, kufanikiwa kivipi?

Tatizo binadamu ni wabishi sana…

Cc: @Mahondaw

Neno kuntu
Nalog off

Kwani wewe unalielewaje neno ‘kufanikiwa’? Labda tuanzie hapo…