JINSI YA KUPIKA VITUMBUA

JINSI YA KUPIKA VITUMBUA

:diamonds:MAHITAJI

Mchele kilo 1

Nazi kubwa 2

Hiliki kiasi

Sukari robo kilo

Hamira kiasi kijiko kimoja nusu ( itategemea aina ya hamira)

Mafuta nusu lita

:diamonds:JINSI YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

  1. Uloweke mchele uliokwisha uchambua vizuri na kuupeta.

  2. Utandaze sehemu safi ukauke, kisha usage upate unga mlaini

  3. Kuna nazi uchuje tui zito

  4. Saga hiliki, changanya na sukari

  5. Changanya ule unga wa mchele, sukari, hiliki, tui la nazi na hamira. uvuruge uwe mwepesi kiasi cha kuweza kuchoteka kwa upawa.

  6. Acha uumue kwa dakika 25 hadi 30 kutegeme na ubora wa hamira.

  7. Weka kikaango cha kukaangia vitumbua jikoni, anza kukaanga vitumbua vyako kwa kueka mafuta kwanza yapate moto, kisha unachota kwa upawa unga na kueka kwenye vijungu vya kikaangio chetu.

  8. Acha vichemke upande mmoja, kisha unageuza upande wa pili, vikishaiva vitoe weka kwenye chujio ili mafuta yajichuje.

  9. Endelea kukaanga viliobakia mpaka unga uishe.

  10. Ukivipata vya moto moto na chai pembeni vitakukosha sana

NB ; NAZI NI KWA AJILI YA KULA KiFAMILIA UKIPIKA KWA AJILI YA WATEJA UTAKULA HASARA . MASOMO YETU YOTE NI BURE KABISA
Follow
@JinsiYaKupika

hii ingevutia zaidi kama ingekuwa video.

Kabisa kabisa

Watu ya bandoz ndio iko mingi hapa so,no,no videos:D:D

:p:p Nimekuelewaa Mkuu