Kama una stress pitia hapa, usiache na wewe kutupia maneno yako!!!

#1
Huku tukiendelea kupunga upepo huku kwa majirani zetu, tuendelee kupata burudani na kutoa stress kwa huu uzi wetu pendwa...

Leo kidogo nipigwe na MWANAMKE baada ya LIFTI kusimama...wakati tupo kwenye lift Nilikua nayaangalia MAZIWA yake akasema "Bonyeza Moja"mi si nikalibonyeza?
Yaani had sasa
bado najiuliza nilipokosea.


Hivi Utajisikieje Utakaposikia Rafiki Yako wa Karibu Hajaja Kwenye Mazishi Yako ???!
Nadhani Mimi Sitamwongelesha Tena !!!
I think nakaribia kupona

Nimenunua chips ili nile kwa bahat mbaya mtoto wa mama mwingine amekaa next to me akaanza kuzililia.
Imebidi nivae earphones. Napenda watoto, ila utoto ndio sipendi..


Jana nimepita njia ya mkato makaburini warembo wawili wakawa wananikimbilia wanatetemeka Eti tunaogopa kupita peke yetu na mm Nikawajibu hata mm nilivyokuwa hai nilikuwa naogopa sana . Wakazimia
Sipendagi kufatwa fatwa m
 

Ntolilo

Village Elder
#20
Customer Care ya Wadada wa Saluni za kiume iko juu sana....yaani anaweza hata akakuchanganyia upupu kwenye Scrub na muwasho ukausikia ukiwa nyumbani!.. hapa unaweza hata kubandikwa lami ya strabag kwenye kipara na bado ukahisi ni easy wave!.

Kuna ile kitu inaitwa Massage ya kichwa,...aisee hapa hata uwe Jenerali wa jeshi lazima utakuwa mpole kama anaungama!,...yaani unakuta mtu kasinzia anakandwa utosi huku analamba midomo kwa raha kana kwamba kapata Scholarship ya kusomea Gesi huko Freiburg Ujerumani!.

Unaambiwa "Kaka tukupake na dawa ya mba?..NDIYO NIPAKE....je Scrub ya Maboga ?"...unajibu tena NDIYO".....hujakaa vizuri unasikia "tukuwekee Tango kwenye Kidevu?"......Unajibu NDIYO!'....halafu unasikia tena "Tukupake Limao kwenye Upara?...hapa napo jibu ni NDIYO kana kwamba unapokea ufunuo!

*Mwisho wa siku unaletewa Bili laki moja na thelathini na tatu-133,000/-!.....na hapo sasa ndipo unapomuona Bwana Israel mtoa roho ameketi jirani yako nae ananyolewa kiduku..!*
 

Top