Kauli za Spika Ndugai na hatima ya Tanzania

Gazeti la Mwananchi, leo 27 Juni 2018 limemnukuu Spika wa Bunge la Tanzania; Job Ndugai ametoa kauli inayoashiria kuwataka Mawaziri kuyatenga kimaendeleo majimbo ambayo Wabunge wao hawakuunga mkono bajeti zao.

"Mawaziri tuwakumbushe, sio upewe bajeti na hawa ukawatumikia hawa, " alisema huku akicheka. “Huwezi kukataa bajeti halafu unakuja kuuliza una mpango gani na daraja langu, sasa bajeti si uliikataa.”

Source: Mwananchi 27 Juni 2018.

Hii sio mara ya kwanza kwa Spika Ndugai kutoa kauli ya aina hiyo inayoashiria kuyatenga kimaendeleo majimbo yenye Wabunge wa upinzani. Kauli za aina hiyo hazikuwahi kutolewa na Maspika waliomtangulia: Mzee Sitta na Makinda. Ndugai ameamua kujiiongeza mwenyewe na angependa kuona Watanzania waliochagua wabunge wa vyama vingine wanatengwa na sehemu nyingine za nchi. Kwa kauli hizi , huko tunakoelekea tusishangae baadhi ya Majimbo kudai mamlaka ya kujitenga na kuunda Jamhuri (nchi) zao.

Kauli ya Ndugai inaashiri udikteta na uminyaji wa demokrasia na maoni ya watu wenye mawazo tofauti, huko tuendako tusije kushangaa yakitokea hayo.

Kaka

Hii sio

Hii Kitu hii

Hizi kauli ni hatari sana kwa usalama wa Taifa, ila kwa sababu ya ulevi wa madaraka basi wanajitamkia lolote linalowajia mdomoni bila kujali athari zake.

Kuna siku baadhi ya mikoa ama majimbo yatagoma kulipa kodi kwenye serikali kuu kisa kutengwa mgao wa serikali kuu.

Tungeweka utaratibu wa kisheria wa namna ya kupeleka hizi pesa za maendeleo wilayani. Haya mambo ya maendeleo kupelekwa sehemu kwa matakwa ya waziri au Rais ni hatari.

Asamehewe tu huyu mla viwavi, ubongo wake una funza.

Inashangaza hakuna mtu anasemea wala kukemea. Ngoja tusubiri wanaharakati, labda watalikemea.

Hizi kauli sio ngeni kutolewa na Ndugai pale Bungeni , mara ya kwanza alisema na hakuna aliyekemea na jana amerudia tena kwa kuwa awali hakukemewa na sasa inaelekea kuwa kawaida.

Kaka

kama wanalengo la kuigawa nchi kwa kufuata itikadi za vyama na wafanye hivyo kisha wauone mwisho wake! mpumbavu mkubwa huyo ndugai, na soon atarudi India kenge huyo

Hii nchi mambo ni mengi

ndugai ni kilaza,wala msisikilize,awaambie na TRA wasichukue kodi kwenye majimbo ya wapinzani,sio wakimbilie kuchukua kodi halafu wananchi wabaguliwe ktk kupata maendeleo

Hiyo point ya msingi

Kama anataka kuwanyima pesa za maendeleo, kwa kuwa wameikataa bajeti, nasi na asichukue kodi kwa wahusika

Lakini tusimlaumu Spika, uwezekano mkubwa ni kuwa maneno hayo katumwa kuyasema na huyo Bwana Mkubwa aliyeko Ikulu, ambaye yeye kuligawa Taifa hilo kwa misingi ya itikadi za kisiasa ndiyo “policy” yake!

Hivi hujaona wabunge wakitokwa na mapovu kutokana na Sera hiyo ya kuingiza pesa zote hazina??

Halafu unyenyekee kwa Waziri au Katibu Mkuu, ambaye ni mtoto wa Dada yake Magu, halafu utegemee “hisani” za hao mabwana wakubwa kama wataleta pesa ya maendeleo jimboni kwako!

huyu jamaa mgonjwa kabisa…

Kauli hizi zitamtafuna siku moja!

Tutadai haki ya kutolipa kodi pia. Nalipia kodi kitu gani sasa kama huduma stahiki sipewi?

Atapata tabu sana.

Hajui cheo Ni dhamana Ni Muda Tu atakuepo mwingine Yeye ashastaafu

Ndungai ni kilaza

Hii inaonesha ni jinsi gani tumeshuka katika viwango. Ndugai na Tulia na Anne Makinda wote walitumwa kuudhibiti upinzani bungeni. lakini Makinda alikuwa anajiongeza kwa kujenga Chemistry na upinzani. lakini ukiangalia Tulia, ni bomu la kutoa machozi. Ndugai kuna wakati anajishitukia, kuna wakati anauma na kupuliza. ila Tulia ndio kabisaaaaa hana msalie.

Shida kubwa ni kwamba wote wanashangilia utadhania mazuzu vile. wako tayari kutumia fimbo yoyote ile kuupiga upinzani. kupinga bajeti ya serikali ni kutumia haki ya kidemokrasia, ili mabadiliko yanayotakiwa yafanyike. tunaambiwa hii ni nchi inayofuata Demokrasia, tena ya Vyama vingi. hizo ndio principles zake. sasa ukianza kusema wanaopinga bajeti majimbo yao yasipewe fedha, unataka kusema hii ni nchi ya chama kimoja? au kupinga kitu ni kuvunja sheria? inaonekana Ndugai ana matatizo katika ubongo wake, na ni mbaya zaidi kuliko hata Magufuli

Enzi hizi hakuna sheria inayofuatwa. Tulikotoka ni kubaya, tunakoelekea ni kubaya zaidi.

Kauli za Viongozi tumbo zitaisambaratisha nchi yetu penwa hivi punde.