Kesi ya Kangi Lugola na wenzie kuomba rushwa iliishia wapi!?

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imekamilisha upelelezi wa kesi ya rushwa inayowakabili wabunge watatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wabunge hao wa CCM ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ni Ahmed Saddiq (Mvomero), Kangi Lugola (Mwibara) na Victor Mwambalaswa (Lupa).

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Godliver Kiriani aliiambia mahakama ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na aliomba ipangwe tarehe kwa ajili ya kuanza kuwasomea washtakiwa maelezo ya kesi inayowakabili.

Hakimu Simba alipanga kesi hiyo ianze kusikilizwa Julai 4 baada ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Washtakiwa hao ambao hadi jana hawakuwa na mawakili, wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Sh5 milioni.

Wabunge hao walipandishwa kizimbani na Takukuru kwa mara ya kwanza Machi 31, 2016 na kusomewa mashtaka na wakili wa Takukuru, Maghela Ndimbo.

Washtakiwa hao wanadaiwa kwa nafasi zao za ujumbe wa LAAC, waliomba rushwa ya Sh30 milioni kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro, Mbwana Magote ili waweze kutoa mapendekezo mazuri ya Taarifa ya Hesabu za halmashauri hiyo za mwaka 2015/2016.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo, Machi 15, 2016, kinyume cha kifungu cha 15 (2) cha Sheria ya Takukuru, wakiwa katika Hotel ya Golden Tulip, iliyoko eneo la Masaki, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 1.JPG

Je, walikingiwa kifua kama ilivyo kawaida ya MACCM kulindana kwenye maovu yao? Ni nani aliyewakingia kifua? Je, TAKUKURU wanaweza kuulizwa kesi hii iliishia wapi!?

Kwa sasa Lugola kapanda cheo unadhani kuna lolote hapa…

Hii kesi najua ishakatwa kichwa toka zamani tu

Naam najua hilo Mkuu hawa wezi na mafisadi wanavyokingiana vifua kwenye mauvo na madhambi yao chungu nzima dhidi ya Watanzania. Sheria za nchi zingekuwa zinafanya kazi vile inavyotakiwa wote waliomo ndani ya hii Serikali na CCM wangekuwa lupango kwa maovu yao mbali mbali.

Itakuwa walishinda na sasa “ameinuliwa”

Ilifutwa kwa madai mepesi ya kwamba serikali (TAKUKURU) hawakuona sababu ya kuiendeleza.

Wezi na mafisadi hukingiana kifua kila siku. Kumbuka ile ya Kikwete ya kulivua gamba na hivyo kuwafukuza “mafisadi” wanaokichafua” chama. Wakamtisha kwamba wewe Kikwete si msafi tutaanika uozo wako wote ikiwemo kampeni zako chafu za 2005 kuwania Urais akanywea na hakuna gamba lililovuliwa.

http://www.liberatetanzania.com/

abeeee??? Mweh

Hujambo weye BT?

Hiyo kesi ndo ishakufa kifo cha mende…

Mpaka maagizo yatoke juu… tuvuteni subira…

Cc: @Mahondaw

miss you ujue