Karibuni nyote nikitumai kuwa mola kawajalia kuiona siku ya leo.
Nawashukuru @Kamu na @123tokambio kwa kuendeleza mjadala ambao un dhana ya kutusisismua na kufahamishana.
MISAMIATI YA LEO
-[B]Goldsmith…Sonara
-Blacksmith…Mhunzi au Mfua Chuma au Mbini
-Engineer…Mhandisi
-Mason …Mwashi
CHEMSHA BONGO [/B]
[B]i)Blackmarket…
ii)Accountability…
iii)Install…
iv) Surf(the internet)…
v)Workshop…
vi)Sycophannt…
vii)Maana tatu au zaidi ya neno ‘Paa’.
Accountability siyo utandawazi. Install bado. Umejaribu hayo mengine lakini maana ya tatu ya Paa elezea bila kutumia neno Paa kama alivyoelezea kaka mkubwa @gashwin.
Sijapatana na jina lake maalum lakini yuajulikana kwa kazi yake. Kwa hivyo yuaitwa 'Mwigaji wa ngono maarufu’ au ’ Mwigishaji wa filamu za ngono maarufu’.
i)Blackmarket… soko haramu
ii)Accountability… uwajibikaji
iii)Install…sanikisha
iv) Surf(the internet)… (hili silijui)
v)Workshop… karakana
vi)Sycophant… (hili pia linanipiga chenga)
vii)Maana tatu au zaidi ya neno ‘Paa’.