Kiswahili endelevu

Natumai mola ametukirimu afya njema Siku ya leo wanakijiji wapenzi.Twaomba leo iwe siku yenye ufanisi teletele kwa kila mja mwenye nia njema.

MISAMIATI YA LEO
-Pangolin- Kakakuona
-Tranparency- Uwazi
-Taskforce- Jopokazi
-Activist- Mwanaharakati (kwa mfano @Okiya )

CHEMSHA BONGO

Tafsiri maneno yafuatayo:-
i) Yardstick…
ii) Ethics…
iii) Doll(child’s toy)…
iv) Remote Controller(the gadget)…
V) Bainisha kati ya Moyo na Roho.
Vi)Maana tatu au zaidi ya neno ‘chungu’.

Shukran.

Doll = kikaragosi

Chungu,1. Hisia isiyopendeza na la kuumiza, 2. Kipande cha mmea mtama inayoshikilia mbegu, 3. kitu inayo onja kali mdomoni,
Moyo na Roho, Moyo ni heart na roho ni soul

i) yardstick-kigezo
ii) Ethics-maadili
iii) Doll-mwanasesere
iv) Remote controll- rimoti udhibiti
v) moyo
roho- kiungo muhimu kwenye miili ya bwanyama na binadamu cha “kupiga” damu miilini
vi) chungu-kali kwa kuonja
-mingi
-chombo cha kupikia

puppet/sycophant-kikaragosi

ok, i thought they shared the same meaning.

[ATTACH=full]49945[/ATTACH] alafu mbona google iko sallow hivyo ati fridge kwa kiswahili ni friji …

Chungu

1.ile ya kupika
2.kitu kuwa kali
3.Mdudu

Moyo-heart…Hichi ndo Kiuingi Mwilini

Roho-Soul-Hii ni nafsi iliyo ndani ya mwanadamu

Okay

Moyo na Roho, Moyo ni heart n a roho ni soul ha ha Bure kabisa tumia swahili

Janjaruka kaka… GIGO
[ATTACH=full]50010[/ATTACH]

iv) Remote Controller(the gadget)…Kitenzambali
(Sikuwa na habari pia, imebidi nichimbe kwenye kitabu changu:))

Sivyo.

Vyema kabisa.

Umejaribu lakini umekosea maana moja ya neno Chungu. Kisha kubainisha kwako kwa Moyo na Roho kuko sawa lakini tumia Kiswahili.

Hapo sawa kaka isipokuwa tu 'Remote controll na maelezo ya Moyo na Roho. Hongera.

La hasha.

Kwa mara nyingi mtandao hauna maneno ya kiswahili sahihi.

Hapo sawa kaka. Kongole.