Allan wahsalan ni ijumaa nyingine njema tumewezeshwa kuiona na twashukuru. Tutajizatiti kwa hali na mali kuendelea kuyanoa Makali ya uweledi wetu wa lugha ya Kiswahili na pia vilevile kutandua tanda bui kwenye bongo zetu.
Msamiati wa Leo
-Cobweb…tanda bui au utandu wa buibui
-Maize Cob…Gunzi na sio ‘msogoro’ kama tulivyokuwa tukiita tukiwa wadogo.
CHEMSHA BONGO
Tafsiri maneno haya;
i) Nauseau…
ii) Wink………
iii) Mirage…
iv) Honeymoon…
v) Elezea ‘miziki ya ala’ ni miziki aina gani?