Kiswahili endelevu

[B]Tuchukue hata ikiwa punje ya sekunde kumshukuru mola muumba wa vyote vilivyomo duniani na hata mbinguni kwa hino siku nyingine aliyotuwezesha kuiona.
Uzi huu wetu wa Leo utakuwa mgumu kiasi kwa wale walikuwa hawaenzi somo la isabati au hesabu wakati walimokuwa shuleni na vyuoni lakini ni vyema kujaribu kwa sababu mswahili alisema ‘kupotea njia ndiko kujua njia na usilolijua tu ni usiku wa giza!’

MSAMIATI WA LEO

AKISAMI
-Akisami ni nambari inayowakilisha sehemu fulani ya kitu kizima(fraction).Katika Akisami, ni lazima pawepo nambari ya juu na ya chini na huyenganishwa na kijistari cha alama ya mkwaju au mlazo(/).
Kwa mfano: 1/2 (one over two or half ) huitwa nusu.

CHEMSHA BONGO

Akisami zifuatazo zaitwaje kwa kiswahili?
i) 1/3………
ii) 1/4…
iii) 1/5…
iv) 1/6…
v) 1/7…
vi) 1/8…
vii) 1/9…
viii) 1/10…

‘Makambo ezali minene!’ Kwa kilingali ni kumaanisha ‘Mambo ni makubwa!’

Shukran wangwana!.
[/B]

Ebu nieleze wanasema nini kwenye wimbo huu naoupenda sana

https://www.youtube.com/watch?v=FbVX4gXPFWY

najua thuluthi na robo…ah, na kifungu cha kumi…

[B]i) 1/3……… Theluthi/thuluthi
ii) 1/4… robo
iii) 1/5…humusi
iv) 1/6…sudusi
v) 1/7…subui
vi) 1/8…thumuni/ thumni
vii) 1/9…tusui
viii) 1/10…ushuri

Shukran[/B]

@xuma asante sana.
I have a class 8 boy who thinks I am a genius because of you.

@123tokambio karibia Kiswahili funzo

Sijawahi ona ukijibu lolote hapa. Kwani kiswahili chako kina kasoro?
Keti pale-------------------------------------------------->

Hata wewe keti paleeee---------------------------------------------------------->

Umbatanishi.

Woi!!!.. @xuma kuja unifafanulie hii sentensi…

Haha naona
Uko makini.

Sasa adviser inakujia wapi kwenye mazungumzo ya wadau wa kiswahili? Wewe hujiita Mtanzania, ila huonekani kwenye mazungumzo ya kiswahili. Ni domo domo za siasa tu; ambazo pia huziezi…

Nipate kwa jukwa la ki maendeleo . Hapa @xuma yupo nami sinajukumu
Lingine

:D:D:D:DUsiwe unakosa kuhudhuria masomo basi.

Nitakupa kaka tegea idhaa hii.

Kongole kwa kujaribu kwa kuwa umepata za kwanza mbili.

:D:DLeo @123tokambio na @Mtanzania Magufuli mmenoana vya kweli.

[B]MAJIBU YA LEO
Akisami zifuatazo zaitwaje kwa kiswahili?

i) 1/3………theluthi au thuluthi: kongole @gashwin na @bababibitoto
ii) 1/4…robo: kongole twna @gashwin na @bababibitoto
iii) 1/5…humusi
iv) 1/6…sudusi
v) 1/7…subui
vi) 1/8…thumuni au thumni
vii) 1/9…tisau au tusui
viii) 1/10…ushuri[/B]

Hongera @bababibitoto kwa kuyapata maswali yote kwa usawa. Nilidhania yatakuwa kizungumkuti kwa wengi kumbe sivyo.Shukran kwa wote walioshiriki na hata @The_Virus nitakushughulikia pamoja na wapenzi wengine wa miziki ya lugha ya lingala.

[B]Msemo wa siku: Akumulikaye mchana, usiku atakuchoma!

[/B]

Lokua Kanze did a good job in this song.He is a renown writer and singer. The lyrics are long but I will give you a summary of the whole thing and later post a translation of the song word for word.

Aaa ma ma ma maah,
Nakeyi kasi lobi nakozonga,
Lobi nakozonga,
Mobembo ezali nde liwate oooh,
Nakeyi kasi lobi nakozonga.
Bayamaah,
Mobembo ezali nde liwate oooh,
Blablablabla …to be continued.
Nakozonga means ‘Nitarudi or I will return’.
In the song Lokua is telling his beloved that
Naondoka leo kwenda kutafuta maisha bora (kufanya kazi katika nchi nyingine majuu) lakini nitarudi. Ninasafiri,sijakufa. Siku za usoni nitarudi kwenye nchi yangu.Nchi nilizaliwa kwa sababu kuna kuumia kwingi kwenye hii nchi ya wenyewe…
Natumai uko sawa @The_Virus .