Kiswahili endelevu

Ahlan Wahsalan ndugu zangu wapenzi kijijini humu.Nina wingi wa matumaini kuwa mu buheri wa afya. Japo nimekuwa kwenye majukumu mengine muhimu, kaka @The_Virus amejukumika kama mwalimu mshikilizi kwa ustadi.

Leo tutaangazia na kujikumbusha misamiati inayoambatana na sehemu zetu za mwili. Kwa mfano:-

-Forehead…Kipaji
-Cheeks…Mashavu
-Chin…Kidevu
-Palate…Kaakaa
-Gum…Ufizi
-Adam’s Apple…Dundumio/Kikoromeo/Kongomeo/Zoloto

CHEMSHA BONGO
-Elezea sehemu hizi kwa kiswahili sanifu.
i) Rectum…
ii) Appendix…
iii) Ankle…
iv) Sole/Footprint…
v) Fistula(a crack in the sole of the feet)…
vi) Fistula(Medical problem associated to women)…
vii) Shin…
viii) Cleavage(…that gap between a woman’s breast)…
ix) Fracture…
x) Sperm…

Natarajia @uwesmake alijibu swali nambari kumi kwa sababu yeye ni mweledi wa ‘kukamua nyoka’. Magwiji wengine kama @Mjuaji , @123tokambio ,@bababibitoto , @Chifu ,@introvert ,@mukuna ,@Meria Mata ,@gashwin , @The_Virus ,@It’s Le Scumbag na wengineo karibu.

Methali ya leo: Joka la mdimu hulinda watundao!
Shukran.

[B]

[/B]

Ahlan wa sahlan:D
Wacha nifungue ukurasa kwa kujaribu hili neno
iv) Sole/Footprint… Wayo

Hapa nami najua tu kisigino.

Rectum - mkundu/puru

Tafsiria anko uwes momo kwa kiswahili kwanza!

Sperm = mbegu

Brother @xuma, my son is sitting KCPE this year. I told you once that he thinks I am a genius…because of you.
Hardest part of my day is when he gives me an insha to read.

Hehehe… I can relate… Hizo misamiati, tanakali za sauti, methali na vile wao hu describe morning vile waliamka, wakapiga mswaki etc gives me a migraine

Shait.
I read once ati nilidamka dem dem.
The Jaruo in me tucked tail…

Sperm-shahawa/manii

Shahawa/manii ni semen/cum…i stand to be corrected though

i) Rectum…mjiko
ii) Appendix…kidole tumbo
iii) Ankle…kifundo cha mguu
iv) Sole/Footprint…wayo
v) Fistula(a crack in the sole of the feet)…pass
vi) Fistula(Medical problem associated to women)… Pass
vii) Shin…muundi
viii) Cleavage(…that gap between a woman’s breast)…pass
ix) Fracture…Vunjika
x) Sperm…Mbegu ya kiume

Sivyo kaka.Mkundu au kinyo (ashakum si matusi) no Anus kwa kiingereza.Jaribu tena.

Mbegu za aina gani?

Hilo si jina la kiswahili lakini hutumika kuashiria ukubwa wa kitu hasa wanawake walionenepa.

Ningeweza kumnoa Makali kupitia kwako kama ningeweza kuziona insha zake.
Cha msingi na cha muhimi sana kwenye uandishi wasinsha no kuhakikisha ana mtiririko mzuri wa maelezo yake unaofuatilizia mwelekezo wa maelezo yake. Wanafunzi wengi hukimbilia misamiati na misemo lakini ukisoma insha zao hazina mtiririko ambao waelezea mantiki ya aina yeyote.

Insha ikiwa na mtiririko mwema,hapo sasa waweza kuirutubisha na methali, semi, misamiati, tanakali za sauti na kadhalika.Lakini usiiharibu kwa kuzidisha kwa sana.

Asan

Asante.
Nitakuinbox insha moja…

Fistula (crack in the sole of the feet) -Makenye.

Mbegu zalishi

Karibu @Kush yule mnene .Nakubaliana nawe ni mbegu zalishi ; lakini za aina gani?