Kiswahili Endelevu

Ni jumatatu nyingine Mola/Jalali/Rabuka katujalia kuiona. Nina wingi wa matumaini kuwa itakuwa siku iliyoboreshwa naye kwa minajili ya kututunuku kupitia jasho letu linalotokana na kazi ya mikono yetu.

Kwenye somo la leo, tutaangazia misamiati inayoambatana na tukio la hivi majuzi lililoshuhudiwa angani la ‘Mwezi kuandamwa’ yaani ‘Lunar eclipse’!

[B]MISAMIATI YA LEO.
-Solar eclipse… Kuandamwa kwa jua au Jua kuandamwa.
-Lunar eclipse…Kuandamwa kwa mwezi au Mwezi kuandamwa.
-Astronomy…Falaki au Unajimu.
-Astronomer…Mnajimu.
-Sky…Mbingu/Anga/Mang’ugume.
-Moonlight…Ubalamwezi au Mbalamwezi au Anga la Mwezi.
-Sunrise…Maawio au Macheo au Matlai au Matlaa au Mashariki.
-Sunset…Machweo au Machwa au Kuchwa au ghurubu au Maghaibi au Magharibi.
-Bright Sky…Kweu.
-Overcast Sky…Mafunde.
-Meteor…Kimondo.

CHEMSHA BONGO:
-Elezea majina haya yanavyojulikana kwa kiswahili sanifu;

i) Planet…
ii) Commet…
iii) Shooting star…
iv) Mercury…
v) Venus…
vi) Earth…
vii) Mars…
viii) Jupiter…
ix) Saturn…
x) Orbit…
xi) Mkusanyiko wa nyota nyingi angani waitwa aje kwa kiswahili?
xii) Alien (jina rasmi la Kiswahili la viumbe midhili ya binadamu vinavyodhaniwa kuishi angani)…

Weledi wa lugha kama kina @mukuna , @123tokambio , @Mjuaji , @Chifu ,@introvert ,@It’s Le Scumbag Scumbag , @The_Virus Virus , @gashwin ,@Meria Mata Mata na wengineo karibuni katika huu mdahalo.

Kumbuka ‘Utamu wa ngoma ni lele!’
Shukrani za dhati! Alamsiki.[/B]

Je unajimu kweli ni sawa na astronomiya ?

OK, jaribio langu hapa.

i) Planet… Sayari
ii) Commet… nyota mkia
iii) Shooting star… nyota bunduki
iv) Mercury…
v) Venus… Zuhura malkia wa angani.
vi) Earth… Dunia
vii) Mars… Mrihi
viii) Jupiter…
ix) Saturn…
x) Orbit…mzunguko wa sayari
xi) Mkusanyiko wa nyota nyingi angani waitwa aje kwa kiswahili? …???
xii) Alien (jina rasmi la Kiswahili la viumbe midhili ya binadamu vinavyodhaniwa kuishi angani)…

Ahlan wa sahlan, nashukuru sana kwa kunialika kwenye ukumbi huu wa kiswahili, wakati ninapojiandaa kwenda kujipumzisha. Kidogo naona jamaa fulani @Mjuaji kesha nitangulia kwa majibu chungu nzima, hivyo basi nitayajaribu machache yaliyobakia, kwa kadri ya uwezo wangu.
vii) Mars… Mihiri
ix) Saturn…Zohari
xi) Mkusanyiko wa nyota nyingi angani waitwa aje kwa kiswahili? Galaksi

:smiley:

Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge

Mmmh… Ya leo ni mawe

planet… Sayari
earth… Dunia
Orbit… Mzunguko
the rest… Nyota mbali mbali

Shukran Zuma kwa mwaliko. Nimekubali mwito wako kwa kujitosa katika huu mjadala. Yafuatayo ndiyo majibu ya maswali uliyouliza.
Planet------------------sayari
Earth-------------------dunia
Saturn------------------zohari
Venus------------------zuhura
Commet---------------Nyota mkia.
Hayo mengine naomba @mukuna aingilie kati.
Shukrani tena.

leo uniweza bwana hakuna ata moja nijuayo hapo:D

Jaribio zuri. Unajimu ni sawa na ‘Astronomiya’ lakini jina ‘Astronomiya’ limetoholewa moja kwa moja kutoka kwa lile la kiingereza.

Jaribio zuri kaka lakini kwa ‘Galaksi’, umenichekesha!

Umejaribu sana.

Wah! Leo umejikakamua vyema kaka!

Usijali kaka. Usilolijua tu ni wakati wa giza. Hapa ni kupashana na kujuzana.

MAJIBU YA LEO
[B]
CHEMSHA BONGO:
-Elezea majina haya yanavyojulikana kwa kiswahili sanifu;

i) Planet…Sayari. Kongole kwa kina @Mjuaji , @4makind na @Chifu kwa kuling’amua hili swali.
ii) Commet…Nyota Mkia. Kongole kwa @Mjuaji na @Chifu kwa kupata hili.
iii) Shooting star…Kimondo.
iv) Mercury…Utaridi.
v) Venus…Ng’anda au ng’andu.
vi) Earth…Dunia. Kongole @Mjuaji , @Chifu na @4makind .
vii) Mars…Mrihi au Mirihi. Kongole @Mjuaji na @123tokambio .
viii) Jupiter…Mshtarii au Sembula.
ix) Saturn…Zohari. Kongole @123tokambio ,@Mjuaji na @Chifu .
x) Orbit…Uzingo au uzungo. Wale walisema ‘Mzunguko’ nimewapa alama.
xi) Mkusanyiko wa nyota nyingi angani waitwa aje kwa kiswahili?..Thureya
xii) Alien (jina rasmi la Kiswahili la viumbe midhili ya binadamu vinavyodhaniwa kuishi angani)…Ajinabu.
[/B]

Shabash! Leo maswali yamekuwa mchongoma kwa wengi lakini shabaha ni kuelimishana na kujuzana. Kama walivyosema wahenga safari ni hatua nasi twaambatana unyo kwa unyo mpaka kilele. Shukrani za dhati kwa walioshiriki na walionakili uwepo wao kama kina @MISCHIEF na wengineo.
Tujumuike katika kipindi kingine panapo majaliwa yake Jalali!
Shukran!

:DThuraya
http://ep.yimg.com/ay/yhst-67029451737615/thuraya-xt-lite-cost-effective-satellite-phone-4.jpg

Simu maridhawa hino. Kuna kusahibiana kwa majina.