Kiswahili endelevu

Baada ya muda murefu wa kupunga unyunyu na kustaajabia mandhari mazuri kwenye kisiwa cha Unguja, kipindi cha ‘Kiswahili Endelevu’ kimerejea tena ulingoni ili tuweze kufahamishana, kusahihishana na kufurahikia nyanja hii ya lugha tunayoienzi.
Somo la leo litakuwa rahisi katika ile hali ya kuutoa ubutu katika bongo zetu.

Munyambuliko wa vitenzi.
Munyambuliko wa vitenzi huhusisha hali ya kutenda, kutendewa, kutendwa,kutendea na kutendana.
Kwa mfano neno:
‘Fanya’ litakuwa- Fanya(kutenda), Fanyiwa(kutendewa), Fanywa(kutendwa), Fanyia(kutendea), Fanyana(Kutendana).

ZOEZI
Nyambua maneno yafuatayo katika hali zote tano.

[B]-Kula-
-Kunywa-
-Piga-
-Pika-
-Lala-
-Tembea-
-Ingiza-
-Andika-
-Tega-
-Lia-
-Bana-
-Kaza-

Kazi kwetu sasa. Karibu wakwasi wa kiswahili kina @introvert , @123tokambio , @Mjuaji , @Eng’iti , @mukuna , @The_Virus , @Meria Mata , @gashwin , @uwesmake , na wale wote wenye ari ya kujaribu.

Msafiri ni aliye bandarini (Meli imeng’oa nanga) Asanteni.
[/B]

6 Likes

Kulana
-Kunywana
-Pigana
-Pikana
-Lalana
-Tembeana
-Ingizana
-Andikana
-Tegana
-Liana
-Banana
-Kazana

1 Like

Hujafwata utaratibu ndugu, lakini umejaribu.

@xuma ntakupa majibu baadaye, saa hii nime shikika kiasi

2 Likes

Asante mdara pumbu/korodani

neno kamua limenyambuliwa kutoka kitenzi kipi?

1 Like

-Kula— kuliwa, kulwa, kulia, kulana
-Kunywa— kunywiwa, kunywa, kunywia, kunywana
-Piga-- pigiwa, pigwa, pigia,
pigiana
-Pika-- pikiwa, pikwa, pikia,pikiana
-Lala-- laliwa, lalwa, lalia, laliana

1 Like

ZOEZI
Nyambua maneno yafuatayo katika hali zote tano.
-Kula- liwa/liwa/lia/lana
-Kunywa- kunywa/nywewa/nywewa/nywia/nywana
-Piga- piga/pigiwa/pigwa/pigia/pigana
-Pika- pika/pikiwa/pikwa/pikia/pikana
-Lala-lala/laliwa/lalwa/lalia/laliana
-Tembea-tembea/tembeza/ tembezwa/tembelea/tembezana
-Ingiza- @xuma pls
-Andika-
-Tega-
-Lia-
-Bana-
-Kaza-

1 Like

Bingwa let me Tell you something boy, nitakutafuta ile ya serious na ntakuvunja vibaya sana msee . F.uck you

Come, I am good both legal & illegal

Vipi mdau @xuma Wacha nijaribu kunyambua haya…
-Kula-
-Kunywa-
-Piga-
-Pika-
-Lala-
-Tembea- Kuendeleza tu kuambatana na @Mjuaji
-Ingiza-
-Andika- Andikiwa, Andikwa, Andikia, Andikiana
-Tega- Tegewa, Tegwa, Tegea, Tegeana
-Lia-
-Bana- Banwa, Banwa, Bana, ???
-Kaza- Kaziwa, Kazwa, Kazia, Kaziana

@mukuna tunakutegea hapa kwenye jukwaa ujiwakilishe…

1 Like

Wacha nijog brain.

1 Like

Limenyambuliwa kutoka kwa neno ‘Kama’. Kwa mfano; Juma anakama ng’ombe.

1 Like

Tumia lugha ya ustaarabu kwenye hili jukwaa kaka.

kwa hivyo itakuwa sawa kusema @Meria Mata Leo anakama import… alafu import (noun) kwa Kiswahili ni?

1 Like

:D:D:D@Meria Mata hivyo asemavyo @Okwonkwo ni kweli?
Kulijibu swali lako, sina jina mwafaka la ‘import’ lakini huwa tunatumia jina ‘maingilio’ ikiwa ni kutokana na kitendo chake. Maingilio ni neno ambalo limekubaliwa lakini huenda kukawa na mengine ambayo nitafanya utafiti halafu nikujibu kwa uhakika.

Jukwaa lina heshma sikatai

Ila, nilomjibu hastahili heshma ya kumzidi nguruwe

Siku nyingi amenibwagia matusi kama jike la ‘wapi senti, nikupe’

Umejaribu lakini umetumia mnyambuliko wa aina moja tu.

Kazi nzuri kaka.

1 Like

Kazi nzuri. Umeboronga ‘Kula’ pekee. Mbona hukuyajibu yaliyosalia?

1 Like

Umepata yale umejaribu isipokuwa ‘bana’.