Kitu ngumu

Nilikuwa nimeanza kuinuka after a lot of life struggles until I noticed a fishy play in Nairobaryy. Utotoni mwangu nimefunzwa kuishi ni kuzingatia na kutia maanani kila kitu naona, kila kitu nasikia na kila kitu napitia. Never appreciated life before ju ya kudhania I was just but a failure (mtu amesoma bila kazi ni nini ingine ka si failure?) . Never knew anything about success lakini pia nilikuja kugundua all my life nimekuwa nikisoma everything about failure. Na hio tu ndio imekuwa ikinipea hope for a better and a good future.
Success and failure ni vitu ziliwekwa kudistracte mwanadamu na mipango za mungu kwa hii maisha. Kwaivyo 2019 was the year of living a Godly life, yani unaishi maisha venye imekuja and to me io ndio nilikuja kugundua ni secret ama niite hidden treasure from the Bible. Nairobi ni shamba la mawe, ndio, lakini nani Alipanda izi mawe? Nani huweka mbolea kwa hii shamba na nani huvuna iii matunda ya mawe? Hahaaa kwaivo ndio nijue exactly what’s this “shamba la mawe” ni nini and the play behind everything ilibidi mimi ka mkulima hodari kutoka western nianze kazi ya kutafta kazi ya Ukulima Nairobi. Guess what? Kwa hii shamba la mawe si ngumu kupata kazi ka mkulima… Mimi uyo nikaamia area code ya molewm Nairobi. Apo nikajuana na uyu msichana wa umri wa makamu, she acted as a shopkeeper with one kid. She looked familiar to me na bila kukosea ni ati nilikuja kugundua yeye ndio hupeana hii kazi ya Ukulima haha.
So after my online job kuanguka I was forced to write a cv na mimi uyooo nikapeleka kwa duka “blessings shop” which by the way ilikuwa misspelled. Haaah dem akaniuliza ka naeza kazi ya mjengo nikamwambia mjengo zii kulingana na mwili yangu, lakini kwa hio mjengo ka Kuna kazi naeza Pata ya mwili yangu mi ni nani? nitaifanya tu, tena si wote kwa mjengo hubeba mawe na kokoto (vitu mzito mzito) naweza Ata kazi ya kumwagilia building maji ikauke pole pole, kuletea watu Chai, uji, kahawa, mandazi(nikaambiwa io ya Chai ni ya madem hahaha, ubaguzi tu) nikamuuliza najee kazi ya gate ama kubeba izo vifaa za mjengo Akina vijiko, gunia na wheelbarrow kuziweka mahali zinafaa.
Maaama yangu! kumbe hii mjengo naambiwa ndio hii “shamba la mawe” naongelelea. Kabla Ata nijue nilikuja kuambiwa kazi nilishaanza note you me sikuwa najua kazi yangu ni gani . Nikirudi nyuma kidogo ninahuhakika kila mtu amewai enda site ya mjengo hapa, mnajua mjengo venye hukuwa. Watu wakoroga watu wa simiti, kokoto, changarau, mawe za building… Foundation ya nyumba watu kuparara na vumbi, matope, simiti bla bla bla na io kwangu haikuwa sheda…si ni mimi tu ndo husema pesa kokoto? Acha ivo Akina Dan na Paulo husema pesa mato? Eee pesa matope… na ka ivo ndo nilikuwa nipate hizi mapesa basi so be it. One week cv ikiwa pale kwa duka aiii nikashindwa tena kunaendaje, maisha imegeukaje sikuizi hadi kazi kwa mjengo haikuji. Nikaamua niaje, wacha niende niconfirm vile Kuna enda kwa Wai-guru wangu wa connections ya mjengo si it’s all about mjengo? Na tena ju ya Ile heshima ya landlady sikuwa nataka end month ifike kama sijapata job. Ule boss akanihakikishia immediately mtu wakupick cv akikuja ataniambia plus pia yeye alikuwa kutafta hio job. Roho ikatulia kidogo kusikia kumbe siko pekeangu haha makosaaaa! Weeky ya pili na ya Tatu ikaingia bila majibu, nikaanza kuregret niaje niliwaste pesa kuenda kutype cv cyber na kazi haijileti Ata after kudrop cv. Izo pesa ningesiaga mahidi zilitoka Ocha io weeky, na the western village elder I am nipikange ugali nikijenga mwili pole pole Ala! Si Ata hio ni mjengo.
Weeky ya Tatu kuisha bado no response. Nika divert akili kwa kitu ingine. Nakumbuka hio siku nilikula muindi two hundred shilling ,nikachangamka marigiti asubui na mapema. Hio siku nilizunguka jiji nikiuzia watu ndizi hahaha by 3pm zilikuwa zimenunuliwa zote,na mimi uyooo nikarudi kejani Nika wash up nikarudi odi wa mtaa. Kumbuka Bado no response kwa Ile story ya mjengo niliambiwa na venye nilikuwa nimejitolea liwe liwalo kazi ni kazi.
End month Kufika ju nilikuwa nalipa rent yangu date ya kwanza kwanza apo nikaamua niaje hio mwezi deposit inisimamie alafu nione vile Imani yangu kwa Uyu mungu mmoja naomba wa Israeli itanipeleka na ukweli nilisimamiwa na deposit yangu na before date 27 mungu alikuwa amenionekania nikapata mpaka doo inaeza nipeleka area code ingine yenye Kuna good internet connection nikarudi online job. First 4 months was good. Rent haikuwa diambo mpaka ikafanya nikaingia kwa bibilia zaidi na zaidi ka Jeremiah hahaha yani sikuwa naamini vile na survive Nairobi ivo kimungu mungu nikiwa na furahia Ile kidogo napata.
Ka tu Ile story ya Job kwa Bible kumbe pia mi shetani aliamua kuenda kuniseti kwa mungu akaamua kutengeza men and women club yake ya roho mbaya apo kando ya ku attack your boy Sokomtu, nikidhani walikuwa wanachangamkia gym daily, prezups kathaa ya vile watanipiga makumbo, masweeps afu mwishowe wanipeleke 6 feets under alafu waende mbinguni kuringia watu wa mungu vile wameniweza. Sa Vile shetani na rende yake walikuja kwangu ata kubisha hawakubisha. Apo ndio kitu ya kwanza kuenda missing ilikuwa simu, plus faiba nilikuwa natumia ikaleta shida tu ivo. Io nikumaanisha mapato yangu ya kila siku ni dead! Nikajaribu sportpesa cyber, mungu wangu! ilinikataa. Uzuri Nyumba nilikuwa nishalipa plus nilikuwa najua maana ya deposit rent just incase nikose namna.
Month haikuwa imeisha Ata, ndio nikagundua this fishy play yenye huchezwa hii Nairobi…ikanileta flashback kwa ule dem nilipea cv na kila kitu nilipitia nikiwa hio area code. So nikiwa base ya jaba note you me mapato haiko na simu iko haiwezi saidia. Nilijaribu juu chini hio mwezi nikaisukuma ivo pole pole pale rounder ya D nikapatana na Mungu akanionesha man cave naeza survival siku mbili ivi and mtaa nikakuwa good. Although naiprove day by day hii game naeza Sema this far ni Mungu na watu wa wikijiji niliinuka Nairobi.

Nimekupea like lakini sijasoma

hii nairobi lazima mtu apitie kitu. ni kama baptism fulani.
mimi kuna time i used to walk hapo pipeline na CD iko na Windows, Office na AV, an star na flat. Nilikuwa technician wa pc so napitia kwa cyber looking for small kibarua huku na kule. 50 to 100 bob if i was lucky. most of the time i wasn’t.

Pole boss. Mungu hawezi kufungia mlango zote, moja itafunguka. Vile nilisema jobs za security, sales ,bar na hoteli zinataka watu kila siku. Zunguka job itajipa

Haina waas @thesavage utapata waks

Na ikajipa tu ivo

It will be well. Trust me