Kufanikiwa unataka ila kuahirisha mambo.

KUFANIKIWA UNATAKA ILA KUAHIRISHA MAMBO!!!
Kuna neno la kiingereza linaitwa PROCRASTINATION. Limenipa taabu sana kulitamka kwa muda mrefu. Linatamkwa
/prokrastineishen/. Yaani, kulitamka tu unaweza kujikuta umeahirisha.
Ulishawahi kujikuta una mambo mengii ya kufanya. Ukajidai unajipanga ili kuanza. Wakati unajipanga unakua unachat kidogo, unaangalia tv kidogo, unapiga simu kidogo…mwisho wa siku ukajikuta hujafanya lolote kati ya mambo hayo. Ukajipa moyo “aaah, ngoja nimalizie movie nitafanya hizi kazi kesho…”
Unatamani kuanza biashara ila toka mwaka jana mpaka sasa unajisemea kimoyomoyo. “Yaani nikipata faida nanunua mzigo mkubwa zaidi…kwani Bakhresa alianzaje…”
Unatamani kusoma ila toka enzi zile unasema. “Nikianza kusoma mie breki yangu ya kwanza PhD”
Unatamani kuoa au kuolewa ila sasa miaka inapita upo tuu. “Huyu akiwa mke wangu…tutakua na watoto wazuriii…na kagari ketu wenyewe”
Huu ni ugonjwa rafiki yangu. Unaitwa PROCRASTINATION. Huu ni ugonjwa wa kuahirisha mambo kwa visingizio mbali mbali.
Napoleon Hill anasema Procrastination ni tabia mbaya, inakufanya mambo ambayo ungefanya juzi unapanga kuyafanya kesho kutwa!! Yaani jambo ambalo lilikua na kila sababu ya kufanywa kabla ya leo limewekwa lisubiri mpaka kesho kutwa.
Victor Kiam aliwahi kusema “procrastination is the assasin of opportunities”. Yaani tabia hii ya kuahirisha mambo ni uuaji wa fursa. Tabia hii itakupotezea fursa nyingi.
Takwimu zinaonesha mtu mzima mmoja katika kila watu watano hua na tabia hii. Na zaidi ya nusu ya wanafunzi wote wana tabia hii.
Tabia hii hupunguza sana utendaji wako wa kazi, hukuletea stress na kuharibu afya yako, hukuletea hofu na kukufanya ujihisi mkosefu kila wakati. Hali hii hupunguza morali wa kujiamini na mwisho kukurudisha nyuma kimaendeleo.
Sababu chache kati ya ulizonazo za kuahirisha mambo ya msingi ni kama vile;
kutokujikubali
kuna wakati unajifunza na kuiga kutoka kwa watu wanaokuzunguka
huna uhakika kama muda ulionao unatosha kumaliza kazi hiyo
huamini kama una ujuzi wa kutosha
huoni sababu ya kufanya jambo hilo kwa kuwa faida yake ni ya muda mrefu
Kuna mtu aliwahi kusema “the best thing to get something done is to get started”. Yaani kama kuna jambo lolote unataka kulimaliza basi ni lazima ulianze. Huwezi kumaliza jambo bila kulianza. Get started!!
Kuna rafiki hupenda kutoa mfano huu; Ukiwa unaendesha gari usiku. Zile taa huonesha kipande kidogo mbele na jinsi unavyosogea ndivyo unaona mbele zaidi. Vivyo hivyo katika maisha. Kama wataka kufanikiwa katika jambo fulani basi huna budi kuanza kwa RASILIMALI CHACHE na muda ulio nao. Jinsi unavyosonga mbele ndivyo utakavyokua na uwezo wa kuweka mambo mengine sawa na mwisho kufikia lengo lako.
Martin Luther King Jr. Aliwahi kusema “you do not have to see the whole staircase. Just take the first step.” Yaani ukitaka kupanda ngazi ndeeefu…huhitaji kuziona ngazi zooote ili ufike juu. Anza na ile ngazi ya kwana na panda moja baada ya nyingine na mwishowe utafika kileleni.
Kama una dhamira haswa ya kufanikiwa basi sitisha na acha kabisaaa tabia yako ya kuahirisha mambo. Karibu tutafakari pamoja leo.

Somo mzuri sana. Mkuu ubarikiwe. Kuna jambo nimeliahirisha. Lamina naghairi kulisubirisha, nalifanya leo

safi sana.

Asante kwa mada nzuri Mkuu.

mkuu hichi ni kitu kinatesa/kinatutesa wengi sana bila kitu kinaitwa commitment ni kazi bure pia wakati mwingine ni kumshirikisha Mungu

Barikiwa pia,Usiliache Fanya leo

Tupo pamoja

Tupo pamoja mkuu

Kwakweli mkuu

Inanihusu 100%

Uanze kuchukua hatua sasa

Mimi nilikuwa na huu ugonjwa kabisaa,.lakini Mungu ni mwema mnoo sasa “ninafanya” na sio “nitafanya”,.Glory to God.

:cool::cool::cool:basi FANYA UKUJE PM…SIKU ILE ULIAHIRISHA, UMESAHAU BABY SHEM?? au na hii utaihahirisha?

Hahahahaa am coming Shem babe…mlango uko wazi lakini?!

Nafanya mkuu

Daaaah hatare sanaaaaa

Babeshem mlango uko wazi…ruksa kabisa kuingia:cool:;):slight_smile:

kama ukweli hivi

Mimi huyu aisee

Hii tabia ninayo kabisa ila naijitahidi kuiacha