Kufuli la mitandao ya kijamii lapasua vichwa wadau wa uhuru wa maoni

Wednesday, June 20, 2018

[SIZE=7]Kufuli la mitandao ya kijamii lapasua vichwa wadau wa uhuru wa maoni[/SIZE]

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/4621480/highRes/2015231/-/maxw/600/-/546jm8/-/pic+mitandao.jpg

[SIZE=5]Kwa ufupi[/SIZE]
[ul]
[li]Utekelezaji huu umeanza kuwang’ata wamiliki wa blogu na mitandao mingine ya kijamii kama Youtube, majukwaa mtandaoni, radio na runinga mtandaoni ambao wamekuwa wakitoa huduma za maudhui mijadala kupitia mitandao.[/li][/ul]
By Tausi Mbowe, Mwananchi
Wiki hii Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeanza utekelezaji wa kanuni za leseni za Sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na Posta za mwaka 2011.
Utekelezaji huu umeanza kuwang’ata wamiliki wa blogu na mitandao mingine ya kijamii kama Youtube, majukwaa mtandaoni, radio na runinga mtandaoni ambao wamekuwa wakitoa huduma za maudhui mijadala kupitia mitandao.
Hatua hiyo imeibua sintofahamu baada ya kuwataka wamiliki wenye leseni za utangazaji wanaotumia mitambo iliyosimikwa ardhini, endapo watapenda kutumia pia kurasa za mitandao ya jamii (Facebook, Instagram na Twitter) kurusha maudhui yao kwa lengo la kuhabarisha umma, kuwa ni lazima nao wajisajili kwanza TCRA.
Tamko la TCRA linasema kanuni hizo zinataka watumiaji wa mitandao hiyo wawajibike kwa maudhui wanayopakia kwenye mitandao hiyo.
Mjadala mkubwa kwa sasa ni jinsi gani mamlaka hiyo inavyotaka kudhibiti mitandao ya kijamii na kuzidi kuminya uhuru wa maoni.
Watu waliozungumza na Mwananchi wameipokea hatua hiyo ya TCRA kwa maoni tofauti, wengi wakiifananisha na “kurudi katika zama za ujima na kukosa uhuru wa kupata habari na kujieleza”.
Wakati Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ngemela Lubinga akiipongeza hatua hiyo, hali imekuwa tofauti kwa waliotoa maoni kutoka vyama vya upinzani, wadau wa habari, wanaharakati na wasomi ambao wanatahadharisha kuwa jambo hilo halipaswi kuchukuliwa kwa wepesi.

Kulinda usalama wa nchi
Lubinga anaipongeza hatua hiyo ya TCRA akisema ni nzuri kwa kuwa inaweka nidhamu iliyo sahihi.
“Kuacha mitandao hiyo iwe holela ni sawa na kuuza nchi na matokeo yake ni kusababisha nchi kuvurugika,” anasema.
Kwa mujibu wa Lubinga, huwezi kuwa na nchi yenye msimamo endapo kila mmoja ataachiwa kufanya anavyotaka.
“Duniani kote ni lazima kuwe na kiasi, kama nchi lazima iwe na msimamo, mamlaka husika zinapaswa kuweka mipaka ya wananchi kufanya wanavyotaka.”
“Wakati mwingine watu wasipodhibitiwa na kufanya mambo kiholela, siku moja wanaweza kupeleka nchi pabaya,” anasisitiza mstaafu huyo wa Jeshi la Wananchi.
Tanzania inarudi katika ujima
Hata hivyo, tofauti kabisa na maoni ya Lubinga, Katibu Mkuu wa NCCR- Mageuzi, Danda Juju anasema hatua hiyo ya TCRA ni sawa na [COLOR=rgb(226, 80, 65)]kuwarudisha Watanzania katika zama za ujima.
Juju anasema kuwa kimsingi uamuzi huo umechukuliwa kisiasa na kwamba ni mwendelezo wa Serikali kuminya demokrasia na uhuru wa kupata habari.
“Huu ni mwendelezo uleule, sasa Serikali inachotaka kuhakikisha haikosolewi na mtu au chombo chochote. Tayari imefanya hivyo kwa vyombo vya habari kwa kupitisha sheria ya vyombo vya habari, wamesitisha Bunge ‘live’ na sasa ni zamu ya mitandao ya kijamii,” anasisitiza katibu mkuu huyo.
Juju anasema endapo watafanikiwa hilo ni wazi kwamba watafanya wananchi wasipate habari za kutosha, lakini pia itasababisha kuwa waoga.
“Unapofungia mitandao ya kijamii unataka kuwa na Taifa la namna gani? Tumeshuhudia mitandao hii ikitoa ajira kwa baadhi ya wamiliki kwani kampuni mbalimbali zinatoa matangazo lakini leo kwa kuifungia ina maana watu wanarudi nyuma,” anasisitiza.

Anasema Taifa lolote linaloendelea linapaswa wananchi wake wawe na nguvu ya kupata habari lakini kutoa maoni na endapo watazuiwa kuzungumza, hiyo ni hatari.
Juju anashauri kuwa njia pekee inayotakiwa ni kuwaacha watu wazungumze na kutoa maoni yao na kwamba Serikali inapaswa kutekeleza yale yote waliyonyooshewa kidole na si kuwatisha wananchi.
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa CUF upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, Abdul Kambaya anasema hatua hiyo ya TCRA inategemea dhamira yake.
“Kama kuna dhamira iliyojificha, siyo sawa maana tumeshuhudia mambo mengi yanafanywa na Serikali lakini nyuma ya pazia wana lengo lao, ni lazima tulipinge hili kwa nguvu zote,” anasema Kambaya.
Anasema mitandao hiyo ina faida lakini pia endapo haitatumika ipasavyo inaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii.

“Kwa sasa kila Mtanzania mwenye uwezo wa kumiliki simu ya kisasa ni mwanahabari, hii inasaidia sana habari kupatikana kwa urahisi, mfano wote ni mashahidi ile habari ya yule mama wa Kilombero, Morogoro aliyejifungua katika kituo cha polisi walianza kuona watu wa kawaida na kutoa habari zake. Kisha baadaye vyombo vya habari vikafuatilia na hatua zikachukuliwa.
“Taifa linahitaji kukua, kuweka vigezo vizito ni kunyima demokrasia na uhuru wa kupata habari,” anaongeza Kambaya.
Hata hivyo, Kambaya anasema kuwa katika uhuru huo ni lazima kuwe na vigezo vyepesi ambavyo vinaweza kuwekwa kwa lengo la kudhibiti watu wasio na taaluma kutoa habari ambazo hazina viwango.
“Pengine TCRA wameliona hili, sasa ni hatari sana kwani kuna habari zinaenda bila kuwa na viwango vinavyostahili na udhibiti, jambo ambalo linaweza kusababisha madhara makubwa,” Anasema.
Kambaya anashauri mamlaka hiyo kuweka vigezo vyepesi vyenye lengo la kuboresha badala ya kuminya demokrasia kama walivyofanya katika masuala ya kuonyesha Bunge moja kwa moja.
Anasema katika kipindi hiki cha utandawazi, mitandao hiyo imeongeza ajira kwa wamiliki wake kwa kupata mikataba ya kibiashara, hivyo kwa kudhibitiwa kutapunguza ajira zilizokwishatengenezwa.

Zuio halina manufaa
Mdau wa habari, Pili Mtambalike anasema hatua hiyo ni matokeo ya kupitishwa kwa sheria mbovu na kwamba kanuni zake hazina manufaa ya kutosha kwa umma.
Mtambalike ambaye ni Meneja programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), anasema kwa kuliona hilo MCT ikishirikiana na wadau wengine, walifungua kesi kupinga kanuni zilizopo katika sheria hiyo kwa kuwa inaenda kinyume na ibara ya 18 ya Katiba.
“Ingawa katika kesi ile iliyofunguliwa Mtwara Jaji alitutaka tukajipange upya, bado sisi kama wadau wa habari tunasisitiza kwamba kanuni hizo hazina manufaa na ndiyo sababu ya haya yote.

[COLOR=rgb(226, 80, 65)]“Nia ya Serikali ni kupunguza uwezo wa wananchi kukosoa waziwazi. Kwa kudhibiti mitandao ya kijamii sasa wananchi hawatakuwa na uhuru tena wa kusema kile wanacho kiamini,” anasema.
Mtambalike ambaye ni mwanahabari, anasema udhibiti huo utapunguza haki ya wananchi ya kupata taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali.
Hata hivyo, anakubaliana na hoja ya Lubinga kwamba kuna athari kubwa iwapo mitandao hiyo itaachwa itumike kiholela.
Ili kuepuka hilo, anasema Serikali inapaswa kuelewa namna ya kukabiliana na changamoto hizo na siyo kama wanavyotaka kufanya.
“Hizi ndiyo athari za mitandao ya kijamii, kwanza huwezi kuzuia ukuaji wa teknolojia lakini pia sasa ni kipindi cha utandawazi, watu wanaotumia njia yoyote kuona moja kwa moja kinachofanyika duniani,” anasisitiza.
“Ni juu ya wewe kama Taifa kujipanga; kuna miongozo mingi inaeleza jinsi ya kutumia kwa manufaa mitandao ya kijamii kwa lengo la kudhibiti na si kukataza,” anaongeza.

Mwanahabari huyo anasema suala la kulazimisha kila mwananchi anayetaka kutumia mitandao hiyo kwa maudhui ya kihabari kulipa mamilioni si sahihi na kwamba hiyo haiakisi hali halisi ya Mtanzania.
Anatoa mfano wa China ambayo imezuia mitandao ya kijamii lakini vijana wake watundu wanatumia kila njia kuwasiliana.
“Sisi tusifike huko tutafute njia bora ya kukabiliana nalo kwa manufaa ya pande zote,” anasisitiza Pili.
Anaitaka mamlaka hiyo kuhakikisha inafanikisha jambo hilo kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa habari na kwamba si jukumu la serikali pekee.
“Mimi kama mdau wa habari hatujashirikishwa ipasavyo, naiomba serikali ijitathimini na kuwashirikisha wadau mbalimbali lengo likiwa ni kuboresha na kupata njia bora.

Matokeo yakuingia madarakani kupitia dirishani, hakuna kujiamini. Ni kuchutama kichakani.

Kabisa Mkuu mtu ambaye anajiamimi na mwenye nia njema na maslahi ya nchi yake KAMWE hawezi kuona tattizo kukosolewa kwa sababu wanaomkosoa hawafanyi hivyo kwa nia mbaya bali kwa nia nzuri kwa manufaa ya nchi na Wananchi wake.

Hivi ile sera ya Kilimo Kwanza - Mapinduzi ya kijani iliishia wapi?

Wahuni hawa Mkuu hawana sera, wanasema kufurahisha baraza tu lakini hawana mikakati yoyote ile. Kumbuka hapa kazi tu kumbe hapa udikteta na ufisadi tu tena mbele kwa mbele.

Madhara ya kuamka asubuhi mkeo anakushauri upuuzi unaenda public unasema Hii ni sheria lazima ipite

KIMENUKA HUKO INSTAGRAM, KUMBE SASA HIVI JOKETI MWEGELO NDIO USINGIZI WA JIWE, BASHITE KAPIGWA CHINI

Jiwe sidhani hata mkewe anamwelewa.

Makubwa hayo!!!

Ila Da Mange jamani!!!

aisee.

Tanzania inapitia kipindi kigumu sana
Nalog off

Wa kusukumizwa at work

Huo ndiyo ukweli halisi na hali ikiendelea kwa kipindi kirefu nchi yetu itaharibika sana na chuki miongoni mwa raia zitakuwa kubwa mno na za kutisha kitu ambacho hakikuwepo Tanzania.

Sugu

Sugu anasema" mpambe anamsifu tajiri mpaka anamshangaa!"
Nalog off

Sugu anasema" mpambe anamsifu tajiri mpaka anamshangaa!"
Nalog off

Haya ndio madhara ya nchi ikiongozwa na mwendawazimu

Mkuu madhara ya kuongozwa na KICHAA hivi sasa ni dhahiri.

Magufool kwenye kiti cha enzi. Shiiiiiit

INA MANA YULE CHEUPE KAPIGWA CHINI NAYE? AMA KWELI TUMEWEKA BEBERU LA MBEGU PALE MAHALI!!

Nimeio

Nimeiona Jana Aisee ila Sidhani kama Kuna ukweli pale