Kuishi nchi yenye Paypal/Stripe restriction ni `hell hell hell` kwa freelancers..

Mimi ni freelancer developer from Tanzania, recently nilipata deal nikalifanya, client akalipa via Paypal… issue ikaja kutoa… nilivyohangaika… hadi natamani kuhama Tanzania kuja Kenya coz ni hell kwa sisi Freelancer devs… hadi narudisha tena kwa aliyetuma atume via bank deposit which client mwenyewe alisema ni process ndefu forms nyingi atatakiwa azijaze also time consuming…

Viongozi always wanacomplain walioelimika wanahama nchini kwao na hivyo hawatumikii nchi yao, so taxes na vingine vingi kwa huyo mtu husika vinakuwa vimeenda nchi nyingine. so kwa case kama hii… mtu akihama still wataendelea kulalamika why walioelimika wanahama nchini kwao…

Nikajaribu pia kufungua paypal as if am kenyan, ikafungua account okay bila tatizo… sababu niliona kenya kuna uwezekano wa kutoa paypal kuja Mpesa(safaricom) na nikawa delighted…
Account niliyoifungua as Kenyan(kwa kuchangua country Kenya) nikawa naitumia kwenye site yangu ninayouza React-Native templates(mobile apps templates) clients wakawa wananunua coz price price yake sio kubwa sana some goes to $50, some to $100.

Pesa ikawa inaingia paypal bila shida na nikajaribu kulipia online ikafanya vizuri bila shida… Nikadhani nimeshinda!!!.

nikapata kazi nyingine nikaifanya, client akataka nimtumie paypal money request, nikaituma kupitia hiyo akaount niliyoifungua as if am kenyan, Paypal wakaituma hiyo request kwa client wangu bila any alert, client akaipata request na akadeposit hiyo $1000 to my kenyan paypal account.

Suddenly, Paypal wakaisuspend my account… they need verification as am kenyan… What the hell… nikajiuliza, hivi even paypal wana loophole ya namna hii… nadhani kama account ina missing information na itakuwa suspended endapo itakuwa deposited kuanzia kiasi flani, why not letting mtu anayetuma hiyo request ajue kabisa account itakuwa suspended sababu kiasi kilichoombwa kimevuka non-verified account limits… wakaruhusu nikatuma $1000 request via their request form na client akalipa kupitia hiyo hiyo form then wakasuspend my account… ningelijua wakati natuma payment request form nisingeendelea sababu nafahamu sina details za kuverify account…

Sikujua kuna kenyantalk… untill today nilivyokuwa natafuta posts za namna ya kuhamia kenya… maybe someone angenisaidia then ningempa kiasi by getting those IDs and nikaverify…
Kazi nilishamtumia client… as soon paypal walivyosema wameverify deposit… and nikadhani nitumie same option as mwanzo kumwambia client aombe refund then niirudishe then atume via bank…
yaliyotokea ni mengine…

For real, Tanzania haitufai Freelancer tunaotegemea online payment na tunaofanya kazi na watu wa nje wanaotegemea kufanya malipo kupitia paypal/stripe etc, coz hawa paypal/stripe etc wanasema country laws haziruhusu wao kufanya kazi zao nchini… and why our leaders wanashindwa kabisa kurekebisha sheria ili hawa guys wafanye kazi hapa tanzania, even mmoja tu angeruhusiwa ili wananchi wake tupate maendeleo…

Not only paypal, even stripe and many others hazifanyi Tanzania but Kenya zipo…
Kenya mpo juu and you will always be the Winner!!!..

Eti deal lilifanya?

Noma jamaa. Pole kwa kazi ngumu. Sasa hela bado zipo suspended ama uliweza kuzipokea kwa namna nyengine?

pole kwa masaibu. As an East African, I think you can easily acquire Kenyan citizenship.

Ahem… Hii baridi inakupekaje??

:D:D:D:DInanimarisaaaaaaaa! Jameni, jana nilitaka kuomba duvet nikapata kombamwiko flani amefunga sanduku la ndani……jinga sana yeye:D:D:D

Watu wa kutoka mbio wanaogopwa

Pole Mkuu…
next timeTumia Payoneer!
Mimi pia sometimes nafanya freelance jobs kama we we, na Clients wengi hawapendi kulipa kupitia Bank sio tu sababu ya kutumia muda mwingi but kwa usalama wa pesa zao…

Client mmoja nikamweleza changamoto za PayPal Tanzania, akanipa idea kutumia Payoneer Master Card, unaweza Ku Withdraw pesa yako anytime any Country, kutumia ATM zinazo support Master Card Worldwide, huitaji kuwa na Bank account…

Mm ndo hutumia hiyo, naweza pia kufanya manunuzi online bila shida.

Hata kule JF nilishawahi kupandisha Uzi kuhusu Payoneer!

Nilimuomba client a request refund then atume via bank deposit… kumbuka nilishampatia project, pesa ikarudi kwake na project anayo hajatuma via bank hadi sasa…

Kabisa… I can’t imagine as a woman kutokwa mbio:D:D

Anaogopa wate, ndio akafunga komplitili :smiley: Sasa ngojeni admin aje ang’oe derailment…

Imagine that! Unaachwa holding the…

Sasa umebaki kupoteza kiasi kikubwa cha pesa. Akikosa kurudisha project waweza kumshtaki kwa paypal?

I wish i could have done that…

Naamini paypal watataka ni verify account kwanza… sababu walitoa timeframe kama sitaupload NationalID yenye majina as yalivyo paypal plus verifying address wanaifunga account… soo bad…

Wacheni kunipiga Makonde jameni, tumpe pole Ndugu yetu anayeumia kutokana na sheria zinazoumiza. [SIZE=2]tiganai nanie[/SIZE]:smiley:

Hapo kweli taabu tupu. Na pia umeshanifunza jambo. Nilitaka kufungua paypal ya pili nikitumia majina tofauti, nchi tofauti, Lakini nimeshaona naweza jipata mashakani siku za usoni… Pole Lakini kwa masaibu uliyoyapata

Pole sana kaka. Izo shida wanazo pia kule Nigeria manake Paypal walirestrict huko after hao ma naija boys kufanya scamming isiyoisha. Hapa Kenya ndio tuna heri kidogo kuna Paypal to Mpesa na pia Paypal to Equity bank. Ulifanya poa kufungua kama Kenyan apo kwa profile lakini haukua makini coz registration na kuitumia pia ulikua unatumia IP address yenye sio Kenyan. Although kuna maninja apa Nairobi wanaweka kukuokolea iyo verification lakini ulitumia njia ndefu. FANYA IVI BOSS sasa rudi kutumia ile yako ya Tz, alafu fungua account ya Payoneer, alafu uandikie payoneer email uwaambie wakupe virtual US bank account ya iyo payoneer yako. Kila payoneer ikonayo. Sasa iyo US bank acc uiweke pale kwa paypal kama your bank account. Sasa withdraw pesa from paypal to your US bank account iyo pesa itaenda kwa account yako ya payoneer. Sasa chukua your payoneer mastercard uelekee kwa Atm yeyote ikona mastercard ukismile na utoe hela yako

Ahsante sana mkuu… ila kwa sasa siwezi update paypal details sababu account imekuwa suspended till niprovide verification… also nilisoma sehemu Paypal hairuhusu kulink payoneer bank details…

Kabla ya Equitybank na Mpesa warahisishe mambo tulikua tunatumia Payoneer. So nko sure inawezekana. Ila kumbuka nmekwambia urudi kutumia ile ya Tz coz ya Ke iko suspended. Ama ya Tz pia imefungwa? Kama bado ipo nenda fanya ivo iyo bank acc ya payoneer itakubali bila ata shida. Alafa sasa ufanye verification. Paypal ukitransact hadi kiwango fulani wanazuia wanaitisha vitambulisho. Ndo manake hiyo ya kenya ikawa ivo. Client angetuma 500 utoe alaf tena 500 utoe hawangefunga maramoja. Sasa coz ulikua mtu wa 50 na miamia then ghafla elfu lazima ingekua ivo. Bots zao wazimu sana. Wamekupa mda gani kuverify iyo ya ke?