Kutumia majina halisi kutaivuruga JF!

Kwanza ni mawazo yaliyochakaa na ya kizamani sana kudhani majina ya kiuandishi (Pen Names) kwenye JF lengo lake ni kujificha kwa mwandishi dhidi ya uovu anaoufanya. Dunia nzima watu wanatumia majina bandia kwenye kazi mbali mbali za sanaa uandishi ukiwemo.

Leo hii ladha ya mabishano ya Kiranga na @Mshana Jr itapungua sana kama watu hao watajulikana uhalisia wao. Majina bandia husaidia sana watu kujadili mada badala ya kumjadili mtoa mada. Lizaboni, Jingalao, @Stroke na wenzao wengine wanajulikana kuwa ni watu wa Lumumba lakini haijulikani ni kina nani. Vipi leo hii Vuta-Nikuvute ijulikane kumbe ni Mwigulu Nchemba?

Kwa mtazamo wangu kujisajili kwa jina halisi iwe ni hiyari na siyo lazima, na ikiwa lazima iwe ni LAZIMA pia kisheria kuomba kibali cha mahakama kufuatilia taarifa za mtu kwenye mitandao ya kijamii na siyo uhuru wa kufanya hivyo waachiwe Polisi. Lazima kuwe na faragha kwenye nchi ambayo kumwita kiongozi Bwege, eti ni kosa la kimtandao!!

Vipi ndiyo vigezo vipya vya jf?

Kwa mujibu wa vigezo vya TCRA!

Nasib Abdul anajiita Diamond inakuwa sawa, ila wana JF kutumia majina ya kisanii inaonekana siyo sawa!

Dah! Naona tutazolewa kama kuku sasa.

aisee kwahiyo tusiite jiwe tuite mtukufu JPM :D:D:D:D:D

Mmmmh aisee mbona kazi ipo

Katika mikutano ya kompyuta huwa kuna kitu kinaitwa ANONYMITY. Hii ina faida zake kisayansi. Inajulikana kwamba mtu akijua nani kasema nini, ataachana na kile ambacho kimesemwa na atashughulika na aliyesema. kwa hiyo ANONYMITY inasaidia watu washughulike zaidi na hoja zilizoletwa badala ya kuhangaika na huyo aliyesema, mke wake, mtoto wake, au hata marafiki zake. Pia kuna tatizo la makundi. inawezekana mfano mtu ni mwanaccm, lakini pia hapendi hili au lile linalofanywa na CCM. sasa akilisema wazi wazi, ataonekana ni msaliti, na watu watajishughulisha kumtukana binafsi, badala ya kuijadili hiyo hoja.

Bahati mbaya sana katika serikali kuna wengi wenye mawazo mgando, kama yaliyotumika kukataa kura ya siri katika bunge la katiba. matokeo yake ndio maana tumekwama mpaka leo. kama ingekuwa kura ya siri pale pangekuwa na adabu na mambo yangekwenda safi kabisa na maslahi ya taifa yangezingatiwa.

Serikali hii ya awamu ya tano imewekeza sana kwenye udhibiti, badala ya kushughulikia hoja zinazozalishwa. na siyo lazima ushughulike na kila kitu. ukisha onekana unashughulikia angalau baadhi ya mambo yanayoibuliwa, utakuwa salama na utasifika kwamba ni serikali sikivu. hofu yote hii inatoka wapi? ndio maana serikali hii inaogopa BUNGE LIVE, inaogopa MAGAZETI HURU, inaogopa TUME HURU YA UCHAGUZI, inaogopa UCHAGUZI HURU.

Tatizo nchi hii tumekabidhi kwa washamba na malimbukeni.
By Zitto Kabwe

Hahahahahaha eti kumuita rais bwege ni kosa kimtandao, rais sio bwege tu ila ni matrako kabisa.

@Mende hawa watu utadhani hawajawahi kusoma kwenye magazeti zilizoandikwa na wale wanaoitwa “mwandishi wetu”. Taratibu itawekwa sheria pia ya kulazimisha na Magazeti nayo yaandike majina yote ya waandishi badala ya kuandika “Mwandishi wetu” kwenye habari wanazoandika.

Lissu alisema hakuna aliye salama!!

khaaa…

!
!
Give Them An Inch They Take Yard,
Give Them A Yard They Take A Mile.
Bob Marley

Kuna Siku Watafunga Internet Kabisa.

Wakikubali tu hilo sharti jf,bora kubakia huku huku kwenye JF ACADEMIA!!

Wewe tulia mbona wewe unatumia Nina halisi
Vyovyote vile itakavyo kuwa sawatu

Mawazo yakishamba hayo

Woga kitu kibaya sana.

Nitakaa huku… let then register it in the US!

Hili kama naliona likianza kufanyiwa mchakato.

laa mkuu punguza hasira